Kupitia taarifa yao waliyoitoa leo Geneva, Uswisi, wataalamu hao wameripoti madai ya majaribio ya mauaji, utekaji nyara, mateso, ukatili wa kingono na vitisho vya kifo dhidi ya wanaharakati wanaofuatilia ukiukwaji wa haki na kusaidia jamii zao. Kati ya Novemba 2025 na Februari 2026, watetezi kadhaa wa haki za binadmau walidaiwa kulengwa moja kwa moja kutokana na kazi yao ya haki za binadamu.
Dawa za kulevya za aina ya Cocaine zanaswa katika Bandari ya Kingston, Jamaika, mnamo Machi 2023.
Ushirikiano wa kimataifa kupitia mikataba ya kimataifa ya kudhibiti dawa umesaidia watu duniani kote, imesema hii leo Bodi ya Kimataifa ya kudhibiti dawa za kulevya, INCB wakati ikizindua ripoti ya mwaka 2025 kuhusu hali yad awa za kulevya duniani.
Rais wa Bodi hiyo Profesa Sevil Atasoy amesema, “nchi zimeelewa kwamba njia bora zaidi ya kulinda afya na ustawi wa raia wao na kukidhi mahitaji yao ya kitabibu na kisayansi ni kupitia hatua zilizoratibiwa kwa pamoja. Mikataba mitatu ya kimataifa ya kudhibiti dawa za kulevya, ambayo inaungwa mkono karibu na mataifa yote duniani, inatoa mfumo wa pamoja wa kuchukua hatua za ushirikiano ili kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya duniani.”
Rais wa zamani wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, (kwenye skrini) anaonekana mara ya kwanza katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko The Hague mnamo Machi 2025.
Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte
Na leo ikiwa ni siku ya tatu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huko The Hague Uholanzi kuthibitisha iwapo kuna ushahidi wa kutosha wa kumfikisha mahakamani Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte kwa madai ya uhalifu dhidi ya ubinadamu unaohusianana kile kilichoitwa “vita dhidi ya dawa za kulevya” nchini mwake, wakili upande wa utetezi, Nicholas Kaufmann amesema hakuna uhusiano uliothibitishwa kati ya hotuba zake za “kipekee, zenye kauli kali” na mauaji anayotuhumiwa kuyafanya.
Wakili Kaufman amesema upande wa mashtaka umeshindwa kuleta ushahidi wa kutosha, na kwa hili, ripoti za mashirika yasiyo ya kiserikali, takwimu za kitaaluma na makala za vyombo vya habari, kwa kawaida, huchukuliwa kuwa hazitoshi.”