Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Ilala imefanikiwa kudhibiti kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 baada ya Kufanya uchambuzi wa Mfumo wa uwasilishaji wa michango ya NSSF ya waajiri wa sekta binafsi 71 .
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala Moza Kasubi amesema katika Uchambuzi huo ilibainika kuwa idadi kubwa ya waajiri hawawasilishi michango ya wafanyakazi kwa mujibu wa sheria ya mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa NSSF na baada ya TAKUKURU kuingilia Kati tayari fedha hizo zimewasilishwa katika mfuko wa hifadhi ya Jamii NSSF
(Feed generated with FetchRSS)