Licha ya mabadiliko yake yasiyoisha, upigania haki na usawa huu una lengo moja, kusukuma jamii kuelekea usawa kwa wanawake na wasichana wote na hivyo kujenga dunia yenye usawa zaidi kwa kila mtu.

Wanawake waandamana kupinga ukatili wa kijinsia unaofanywa na wanaume.

© Unsplash/Ehimetalor Akhere Unuabona

Wanawake waandamana kupinga ukatili wa kijinsia unaofanywa na wanaume.

Ufafanuzi wa mtetezi wa haki na usawa wa wanawake 

Utetezi huu ni imani kwamba kila mtu, bila kujali jinsia yake, anapaswa kuwa na haki na fursa sawa.

Ni rahisi kiasi hicho. Licha ya aina mbalimbali za nadharia na vitendo vya utetezi na mitazamo tofauti ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ni msingi mkuu wa utetezi ni kuleta usawa.

Na katika utetezi  wa kisasa unaozingatia mwingiliano wa mifumo ya ubaguzi “intersectionality’’ tunamaanisha usawa kwa wote bila kujali utambulisho wa kijinsia, mwelekeo wa kingono, rangi, tabaka au kabila.

Nani ni mtetezi wa haki na usawa wa wanawake (mfeministi)?

Huyu ni mtu anayeshikilia na kutenda kwa kuzingatia imani kwamba wanawake na wasichana wote wanapaswa kuwa na haki na fursa sawa kama wanaume.

Mtu yeyote anaweza kuwa mtetezi wa haki na usawa wa wanawake.

Watu wanaweza kuwa na sababu tofauti za kuwa /mfeministi. Kama ilivyo kwa majina mengine ya utambulisho, baadhi ya watu hujitangaza wazi kuwa ni watetezi wa haki za wanawake au  wafeministi, ilhali wengine hushikilia maadili ya kifeministi lakini hawatumii jina hilo. Na kinyume na dhana potofu: kumchukia mwanaume hakumfanyi mtu kuwa mfeministi.

“Ni muhimu kuwashirikisha vijana, hasa wavulana, ili wawe mabalozi wa uongozi wa kutetea haki na usawa na kupigania usawa wa kijinsia pamoja na utekelezaji kamili wa haki za binadamu.”- Ishaan Shah, UN Foundation Global Lead Next Generation Fellow

Ishaan Shah, Mshirika wa UN Foundation Global Lead Next Generation

© UN Women

Ishaan Shah, Mshirika wa UN Foundation Global Lead Next Generation

Mtazamo wa haki na usawa wa wanawake unamaanisha nini?

Kutumia mtazamo au lenzi ya kifeministi ni kuangalia suala lolote kwa kuzingatia mienendo ya kijinsia katika maisha ya wanawake yaani, mahusiano ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ambayo mara nyingi huwapa wanaume upendeleo kuliko wanawake.

Kwa nini kutumia lenzi ya kifeministi? 

Kwa sababu kihistoria na hata sasa, kanuni na taratibu za jamii nyingi zimeundwa na kutekelezwa kwa ajili ya wanaume, na mara nyingi na wanaume wenyewe. Huo ndio mfumo dume na unachochea ukosefu wa usawa wa kijinsia.

Mitazamo, mahitaji na mapendeleo ya wanaume huunda mifumo mingi, sheria na kanuni rasmi na zisizo rasmi zinazoongoza maisha yetu:

  • Namna tafiti za kitabibu zinavyofanywa kwa kuzingatia wastani wa wanaume
  • Jinsi mifumo ya akili mnemba(AI) imefundishwa kwa kutumia taarifa zenye upendeleo wa kijinsia
  • Namna kazi za malezi na kazi nyingine zinazochukuliwa kuwa “za kike” hulipwa kidogo au kutolipwa kabisa

Mizania hii isiyo sawa ya nguvu huelemea upande wa wanaume na wavulana. Mtazamo wa haki na usawa wa kijinsia huangalia nani ana nguvu na nani hana – na kwa nini.

“Mazungumzo ya kizazi hadi kizazi na mshikamano wa kifeministi hutuwezesha kwa pamoja kupinga mfumo dume, kujua historia yetu ya pamoja na kusonga mbele.”
— Rabéa Naciri, mwanaharakati wa haki za binadamu na msomi wa masuala ya haki na usawa wa wanawake

Ufeministi unaonekanaje kwa vitendo?

Kuweka mtetezi wa haki na usawa wa wanawake kwa vitendo kunamaanisha kwanza kuwajumuisha wanawake na wasichana katika maamuzi, na kuwawezesha kuongoza katika masuala yanayowahusu. Harakati nyingi za wanawake zimeibuka kutokana na kunyimwa kwa uhuru wao – ikiwemo harakati za kudai haki ya kupiga kura.

Chukua mfano wa kazi za malezi na utunzaji. Watu wanaojali mahitaji ya wengine watoto, wazee, katika familia na jamii hushikilia jamii na uchumi wetu kwa manufaa ya wote.

Rabéa Naciri, mwanaharakati wa haki za binadamu na msomi wa masuala ya wanawake au ufeministi.

© UN Women

Rabéa Naciri, mwanaharakati wa haki za binadamu na msomi wa masuala ya wanawake au ufeministi.

Kuangalia kazi hizi kwa lenzi ya kifeministi ni kutambua kwamba majukumu mengi huwekwa kwa wanawake na wasichana, mara nyingi bila malipo, na wakati mwingine kwa gharama ya fursa zao binafsi na za kitaaluma.

Kuweka utetezi wa haki na usawa wa kijinsia katika vitendo ni kutambua thamani ya kazi za malezi ambayo katika baadhi ya nchi huchangia hadi asilimia 40 ya Pato la Taifa na kuhakikisha wanawake hao wana ushawishi katika sera za serikali na waajiri. Kwa maneno mengine: lenzi ya kifeministi huhakikisha sera zinazingatia mahitaji ya jinsia zote kwa usawa.

Wanawake wanapigania haki sawa

Kwa karne nyingi, wanawake wamepambania haki, fursa na uhuru sawa. Kuanzia wanaharakati wa haki ya kupiga kura hadi wanaharakati wa kidijitali, kila kizazi kimevuka mipaka, kuvunja vizuizi na kukataa kurudi nyuma.

Utetezi wa haki katika historia na tamaduni mbalimbali

Katika historia, harakati za kutetea usawa zimepigania haki ya kijamii na usawa kwa wanawake katika maeneo na tamaduni mbalimbali.

Harakati za awali za kifeministi zilihusiana pia na harakati za ukombozi na uhuru wa kitaifa. Ufeministi haukuwa tu madai ya haki za wanawake pekee, bali pia ulikosoa ukoloni na ukandamizaji, na kuunganisha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Mifano ni mingi:

  • Mageuzi ya kijamii nchini India kabla ya uhuru yaliyoanzisha sheria za kulinda haki za wajane na elimu ya wasichana katika miaka ya 1800
  • Afrika Kusini baada ya uhuru, ambapo Bantu Women’s League mwaka 1918 lilikuwa shirika la kwanza kutetea haki za wanawake weusi
  • Ghasia za wanawake wa Aba nchini Nigeria mwaka 1929 zilizolazimisha mageuzi dhidi ya kodi zisizo za haki

Katika karne ya 19, wanawake katika sehemu mbalimbali za dunia,  kuanzia New Zealand mwaka 1893  walipigania na kupata haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa kitaifa.

Katika miaka ya 1960 na 1970, harakati za ukombozi wa wanawake zilipanua zaidi chaguo za wanawake katika elimu, ajira na maisha ya umma.

Katika miaka ya 1990, utetezi wa kuzingatia mwingiliano wa mifumo ya ulionesha jinsi ubaguzi wa kijinsia unavyounganishwa na kuongezwa nguvu na ubaguzi wa rangi, tabaka, ulemavu, chuki dhidi ya mashoga na aina nyingine za ubaguzi.

Lúcia Xavier, mwanaharakati wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake, ufeministi na ubaguzi wa rangi.

© UN Women

Lúcia Xavier, mwanaharakati wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake, ufeministi na ubaguzi wa rangi.

Leo, utetezi wa haki na usawa unaendelea kukabiliana na changamoto za zamani na mpya: unyanyasaji wa kijinsia, fedheha kuhusu miili, chuki dhidi ya mashoga na watu waliobadili jinsia, pamoja na unyanyasaji wa kidijitali.

“Wanawake weusi ni wahusika wenye nguvu za kisiasa, wenye uwezo wa kubadilisha jamii na kuunda upya kanuni na viwango… Sote tumekuwa tukifanya hivi maisha yetu yote – kutafuta njia za kupinga.” Lúcia Xavier, mwanaharakati wa haki za wanawake na mpinga ubaguzi wa rangi’’

Kwa nini bado tunahitaji utetezi wa kuleta usawa?

Utetezi ni muhimu sasa kama ilivyowahi kuwa.

Duniani kote, wanawake na wasichana wengi bado wanakosa haki za msingi za binadamu. Takwimu zinatisha:

  • Mwanamke mmoja kati ya watatu hupitia ukatili wa kimwili au kingono maishani mwake
  • Msichana mmoja kati ya watano huolewa kabla ya kufikisha miaka 18
  • Matukio sita kati ya kumi ya mauaji ya wanawake hufanywa na mwanafamilia au mwenzi wa karibu

Masuala makubwa ya wakati wetu – amani na usalama, uhamiaji, na ukatili uliokithiri huwaathiri wanawake na wasichana kwa namna tofauti, na wakati mwingine zaidi kuliko wanaume na wavulana.

Ukosefu wa uwekezaji wa kutosha katika takwimu za kijinsia pia hufanya iwe vigumu kushughulikia pengo hili la usawa.

Collage ya picha za kihistoria na za kisasa za wanawake wakiandamana kwa ajili ya haki za wanawake, pamoja na bendera iliyoandikwa 'END FEMICIDE'.

© UN Women

Ushirikiano wa Haki za Wanawake: Ratiba ya Ulimwenguni ya Maandamano

Je, kuna upinzani dhidi ya wanawake?

Kwa sasa, harakati za kifeministi zinakabiliwa na wimbi kubwa la upinzani dhidi ya masuala ya kijinsia. Baadhi ya nchi zilizokuwa zimepiga hatua  ikiwemo usawa wa uwakilishi wa kisiasa na haki za uzazi  zinashuhudia msukumo wa kupinga mafanikio hayo na kutishia kurudisha nyuma haki za wanawake.

Utafiti wa hivi karibuni wa Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake – UN Women unaonesha kuwa upinzani huu unaenda sambamba na kuongezeka kwa harakati zinazopinga demokrasia, ambazo zinadhoofisha haki za binadamu na utawala wa sheria duniani.

Wakati huo huo, ufadhili kwa mashirika ya wanawake umepunguzwa kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni, huku wanaharakati, waandishi wa habari na manusura wakiripoti kuongezeka kwa vitisho dhidi ya usalama wao na familia zao.

“Niliona usimulizi wa utetezi wa usawa na haki kama aina ya upinzani. Ni hadithi za nani zinasimuliwa, na za nani zinafutwa hili limekuwa suala la kisiasa kwa muda mrefu. “Sushmita S. Preetha, mwandishi wa habari wa usawa na haki za wanawake. 

Sushmita S. Preetha, mwanahabari mtetezi wa haki za wanawake.

© UN Women

Sushmita S. Preetha, mwanahabari mtetezi wa haki za wanawake.

Je, wewe ni mtetezi wa haki na usawa wa wanawake (feminista)?

Harakati za haki za wanawake zinahitaji washirika. Je, uko tayari? Hapa ndipo pa kuanzia:

• Jifunze: Panua uelewa wako kuhusu usawa wa kijinsia.
• Tumia lenzi ya haki na usawa wa kijinsia katika masuala unayojali: Fikiria vizuizi wanavyokumbana navyo wanawake na wasichana katika jamii yako.
• Tafuta au unda jamii yako: Historia ya utetezi wa haki na usawa inaonesha nguvu ya mshikamano.

• Tetea: Wahimize viongozi wa serikali, taasisi na biashara kuwekeza katika fursa za wanawake, kulinda haki zao, na kuharakisha hatua za kufikia usawa wa kijinsia.

Tangu mwanzo wake, watetezi wa haki za wanawake wameongoza mafanikio makubwa katika Umoja wa Mataifa, ikiwemo kutambuliwa kwamba haki za wanawake ni haki za binadamu, na kuanzishwa kwa UN Women miaka 15 iliyopita. UN Women inasimama pamoja na harakati za wanawake duniani kote. kwa ajili ya haki na uwezeshaji wa wanawake na wasichana WOTE.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *