Katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva nchini Uswisi, Kamati imesema imeshtushwa na ripoti za mashambulizi dhidi ya miundombinu ya kiraia, ikiwemo shule na hospitali, ambapo mlipuko katika shule ya wasichana ya Shajareh Tayyebeh kule Minab, nchini Iran, unaripotiwa kuua zaidi ya watoto 160.

Kamati hiyo imetoa onyo kali kuhusu usalama wa watoto katika maeneo yenye migogoro ikisema, “Hii ni ukumbusho kwamba watoto ni miongoni mwa watu walio katika hatari zaidi kwenye migogoro ya silaha, na hawapaswi kamwe kutumbukizwa katika vifo vya bila kukusudia.”

UNICEF nchini Madagascar inachagiza haki za watoto kupitia michoro

© UNICEF/Abela Ralaivita

UNICEF nchini Madagascar inachagiza haki za watoto kupitia michoro

Mkataba wa Haki za Mtoto

Mkataba wa Kimataifa wa Haki za mtoto (CRC) unazitaka nchi zote kulinda haki ya kuishi na maendeleo ya kila mtoto, na kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha haki hizo zinaheshimiwa wakati wa vita.

Pande zote zinazopigana katika mzozo wa Iran zimeaswa kufuata sheria za kimataifa ili kuepusha maafa kwa watoto, ambapo Kamati imesisitiza, “Watoto lazima walindwe dhidi ya madhara ya moja kwa moja na yasio ya moja kwa moja ya uhasama. Pande zote katika mgogoro zina wajibu wa kuheshimu sheria za kimataifa za haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu.” 

Wito umetolewa wa kusitishwa kwa mapigano mara moja ili watoto wasiendelee kuuawa, kulemazwa, au kupata madhara ya kisaikolojia.

Kamati imetaka hatua za haraka kuchukuliwa kulinda maeneo ya kiraia hususan shule na hospitali yasishambuliwe, na kuhakikisha watoa misaada wanawafikia watoto na familia kwa usalama. Maelekezo haya yanalenga kukomesha ukiukwaji wa haki za watoto ambao wamekuwa waathirika wakubwa wa mapigano yanayoendelea. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *