#HABARI: Jamii imeaswa kuwalinda watoto ili wasifanyiwe vitendo vya ukatili ambavyo vimekithiri katika baadhi ya maeneo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza katika mashindano ya kusoma qurani Kata ya Vikindu Mkuranga Pwani, mgeni rasmi Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Mkuranga Bi. Tatu Mpeki amesema jamii inapaswa kuwalinda watoto ili waweze kutimiza ndoto zao.

Amesema Serikali imetilia mkazo kuhakikisha haki za mtoto zinatekelezeka kuanzia ngazi ya jamii ikihusisha miradi mbalimbali inayowagusa watoto.

“Si vema kuona mtu mzima akimuingilia mtoto tena wakati mwingine ni mtoto wa kiume kinyume na maumbile hii haiwezekani, ni aibu ni kitendo cha fedheha hakipaswi kufumbiwa macho wala kunyamaziwa tuwe mabalozi wazuri ndugu zangu katika kupiga vita vitendo hivi,” alisema Tatu.

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *