Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar imesema kuwa leo Alhamisi mwezi haujaandama na kwamba Waislamu wanatakiwa kuendelea na mfungo wa Ramadhani.
Taarifa ya Mufti huyo kwa vyombo vya habari imesema kuwa kesho Ijumaa Machi 20 ni Ramadhani 30.
“Hivyo kesho Ijumaa tarehe 20-03-2026 itakuwa mwezi 30 na Jumamosi Machi 21 itakuwa ndiyo mwezi 1 Shawwaal 1447.H.”

(Feed generated with FetchRSS)