Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema kuwa mashambulizi yanayoendelea katika eneo la Magharibi mwa Asia yamevuruga usafirishaji wa baharini na kwamba Beijing itaendeleza juhudu za usuluhishi ili kufanikisha usitishaji vita na kukomesha uhasama ili kurejesha amani na utulivu katika eneo la Magharibi mwa Asia haraka iwezekanavyo.

Lin Jian amesema leo katika mkutano na waandishi wa habari kwamba: Mapigano ya sasa Magharibi mwa Asia yanaendelea kushtadi na kupanuka.

Jian ameongeza kuwa: Mapigano ya sasa yanadhoofisha amani na utulivu katika eneo hilo na yana madhara kwa nishati, masuala ya fedha, biashara na usafirishaji wa meli za kimataifa na kuathiri maslahi ya pamoja ya nchi zote.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema kuwa: Historia na imethibitisha mara kadhaa kwamba nguvu ya kijeshi si suluhisho la matatizo na kwamba mapigano ya silaha yanasababisha uhasama mpya. 

Lin Jian amesema, kwa mara nyingine tena China inataka kusimamishwa oparesheni za kijeshi ili kuzuia hali ya mambo kuwa mbaya zaidi.

Mwanadiplomasia huyo wa China amemalizia kwa kusema: Beijing itaendelea kufanya juhudi za usuluhishi ili kufikiwa usitishji vita na kukomesha uhasama ili kupatikana amani Magharibi mwa Asia haraka iwezekanavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *