Zahran Mamdani, meya Mwislamu wa New York, ametuma ujumbe wa salamu za Sikukuu ya Nowruz na mwaka mpya wa Kiirani kwa Wairani na kutangaza kwamba bado anapinga mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Katika ujumbe wake siku moja kabla ya Nowruz, meya huyo Mwislamu wa New York, amesema: Heri ya Nowruz kwa Wamarekani Wairani wote waliolifanya Jiji la New York kuwa makazi yao!

Mamdani ameongeza: “Nowruz kwa kawaida huwa wakati uliojaa hisia nzuri, lakini mwaka huu hali ni tofauti. Ninaendelea kupinga hujuma ya kijeshi ya Marekani na Israel, na ninawatakia Wairani wote wanaosherehekea sikukuu hii maalumu nyakati nyingi za furaha.”

Awali, Mamdani alikuwa ametaja mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran kuwa ni kinyume cha sheria na yenye matokeo mabaya,” ikiwa ni pamoja na kusababisha madhara kwa raia wa kawaida.

Mashambulizi ya pamoja ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalianza asubuhi ya Februari 28, mwaka huu wa 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *