#MICHEZO: Mvutano kati ya taifa la Senegal na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) umefikia hatua mpya ya kushtua baada ya Kocha wa Senegal, Pape Thiaw, kuripotiwa kulipeleka taji la AFCON kwenye kambi ya jeshi kwa ajili ya usalama. Hatua hiyo imetafsiriwa kama ujumbe mzito na wa kijasiri kwa CAF kwamba taji hilo halitoki mikononi mwa Wasenegali hivi karibuni, licha ya shinikizo la kuitaka nchi hiyo kulikabidhi kombe hilo kwa Morocco.
Inaarifiwa kuwa kombe hilo sasa lipo ndani ya kituo maalum cha kijeshi kikiwa kinalindwa na askari wenye silaha saa 24, ikiwa ni ishara ya “kuzilinda heshima na fahari ya taifa.” Hatua hii ya Pape Thiaw imeungwa mkono na raia wengi wa Senegal ambao wanaona kuwa kunyang’anywa kwa taji hilo “mezani” ni uonevu wa kispoti, hivyo kutumia jeshi ni mbinu ya kuhakikisha hakuna mamlaka yoyote inayoweza kulichukua taji hilo kwa nguvu.
Uamuzi huu unakuja wakati ambapo ulimwengu wa soka unasubiri kauli ya mwisho kutoka Mahakama ya Michezo (CAS). Kwa kuliweka kombe kambi ya jeshi, Senegal inatuma salamu kuwa “taji hili ni mali ya wananchi” na halitarudi CAF hadi haki itakapotendeka, jambo ambalo limezua mjadala mzito kama soka linapaswa kuingiliana na nguvu za kijeshi kwa kiasi hicho.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania