Muigizaji wa filamu za mapigano Chuck Norris amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86, familia yake imetangaza kifo chake katika taarifa iliyotolewa leo rasmi..

Muigizaji huyo wa Marekani alijulikana zaidi kwa nafasi yake katika kipindi maarufu cha televisheni Walker, Texas Ranger pamoja na filamu za mapigano za miaka ya 1980, ikiwemo Missing in Action.

Kabla ya kujiunga na Hollywood, Norris alijijengea jina kama bingwa wa dunia wa sanaa ya mapigano, akiwa na mikanda mingi ya juu (black belts).

kupitia Instagram, familia ya Norris ilimkumbuka kama “mume mwenye kujitoa, baba na babu mwenye upendo, kaka wa ajabu, na moyo wa familia.”

“Ingawa mioyo yetu imevunjika, tunashukuru sana kwa maisha aliyoyaishi na kwa nyakati zisizosahaulika tulizobarikiwa kushiriki naye.”

#kilichoborakabisa

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *