Maafisa usafishaji Manispaa ya Morogoro wameomba Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba kutoa tamko la ukamataji wa bodaboda unafanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini na majini LATRA juu ya faini ya shiling 25,000 inatozwa na mawakala wa LATRA .

Wakiongea na waandiahi wa habari maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda Selestine Agustino, Ramadhani Madunda, Lauliani mgunduzi na Musa Shukuru wamemuomba Waziri Mkuu Mwigulu Lameck Nchemba kutoa tamko la faini ya sh 25,000 inayotozwa baada ya kushindwa kulipa malipo ya 17,000 zinazotakiwa kulipa.

Maafisa usafishaji hao wamesema mawakala hao wa LATRA wamekua wakiwakamata bila kuwa na vitambulisho wala nguo zenye kuwatambulisha kama wao wametumwa kukamata jambo ambalo linapunguza uwaminifu kama wametumwa na LATRA.

Wamesema hata utoaji wanamba ya malipo ( control namba) ya kulipia zimekua zikitoka mbili na wakati mwingine wanaomba wapewe pesa taslim jambo ambalo wanaisi wanaibiwa fedha zao.

Akizungumzia juu ya malalamiko Afisa Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Morogoro, Andrew Mlacha, amesema mawakala wa LATRA kazi yao ya kwanza ni kuoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa leseni ya usafirishaji ya 17,000 na endapo utashindwa kulipa kwa wakati ndipo wanatakiwa kulipa faini ya 25,000.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *