Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20 amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali katika mtaa wa Nyerere, kata ya Ipuli, baada ya kutuhumiwa kumfanyia kitendo cha ukatili mtoto wa miaka saba.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, kijana huyo anadaiwa kumlaghai mtoto huyo kwa kumnunulia pipi na soda kisha kumuingizia uume mdomoni na kumpaka dawa kitendo kinachodaiwa kuhusiana na imani za kishirikina.
Inaelezwa kuwa mara baada ya tukio hilo, mtoto alirejea nyumbani akiwa analia, ambapo mama yake mzazi alimtaka kueleza kilichompata Ndipo mtoto huyo alipofafanua tukio zima na baada ya taarifa hizo kusambaa, wananchi walikusanyika na kujaribu kumshambulia kijana huyo kwa hasira, kabla ya kunusurika kuuawa lakini Jeshi la Polisi likafika eneo la tukio kwa wakati na kumchukua kijana huyo na hapa mtoto aliyefanyiwa tukio hilo,majirani na mashuhuda wa tukio hilo wanaeleza hali halisi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa nyerere kata ya ipuli Manispaa ya Tabora Bw Yassin Hussein anaeleza namna walivyobaini tukio hilo linalohusishwa na imani za kishirikina huku akitoa wito kwa vijana kuachana na vitendo vya uovo na kwamba serikali haitavumilia vitendo hivyo na hatua kali zitachukuliwa kwa yoyote atakayebainika kufanya uhalifu.
(Feed generated with FetchRSS)