Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) imeanza utafiti wa siku 22 katika Ziwa Tanganyika, ukiwashirikisha watafiti kutoka nchi zinazozunguka ziwa hilo ambazo ni Tanzania, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) pamoja na Zambia.

Akizungumza wakati wa Zoezi hilo Mkurugenzi wa Uendelezaji Tafiti na Uratibu kutoka TAFIRI, Dkt. Mary Kishe, amesema kuwa utafiti huo unaofanyiki kwa mara ya pili nchini unalenga kuchunguza mtawanyiko wa samaki katika Ziwa Tanganyika kwa kuangalia tofauti zinazojitokeza kati ya misimu mbalimbali ya mwaka.

Ameongeza kuwa matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kusaidia kuboresha usimamizi endelevu wa rasilimali za uvuvi, pamoja na kuchangia kukuza uchumi wa buluu kwa nchi wanachama.

Utafiti huu pia unatarajiwa kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kwa kuimarisha matumizi endelevu ya rasilimali za maji, kuongeza tija katika sekta ya uvuvi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa buluu, ambao ni mhimili muhimu wa maendeleo ya muda mrefu ya nchi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *