KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amepongeza maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Soko la Bukoba Mjini uliogharimu zaidi ya Sh. Bil 18.9 hadi kukamilika kwake fedha inayojumuisha na ujenzi wa stendi ya mabasi.
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa soko hilo, ambao umefikia asilimia 19, leo Machi 26, 2026 Kihongosi amepongeza juhudi zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanza utekelezaji wa soko hilo, uliotolewa ahadi zaidi ya miaka 10 bila ya utekelezaji na kuanza utekelezaji katika awamu ya Rais Dkt. Samia.
Aidha amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa Soko hilo, Nixxon Kissa, kuhakikisha mradi wa soko hilo ulioanza utekelezwaji wake, Oktoba mwaka huu na kutarajiwa kukamilika January 2027, unakamilika kwa wakati uliopangwa ili wananchi waanze kunufaika nao.
(Feed generated with FetchRSS)