Nchini Kenya, uchunguzi wa miili huko Kericho unaendelea. Kaburi la watu wengi liligunduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika mji huu mdogo magharibi mwa nchi. Vijana, walioajiriwa kama wachimba makaburi na watu wasiojulikana, waliwaarifu polisi. Baada ya kufukua maiti, miili thelathini na mitatu iligunduliwa: watu wazima wanane na watoto ishirini na watano.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu jijini Nairobi, Gaƫlle Laleix

Nchini Kenya, kadiri wachunguzi wanavyoendelea na suhuli yao, ndivyo maajabu yanavyozidi kuongezeka. Kwanza, idadi ya miili iliyopatikana kwenye kaburi la watu wengi ni mara mbili ya waliyotarajia, kwani wachimba makaburi vijana, waliporipoti ugunduzi huo kwa mara ya kwanza, walikuwa wametaja miili kumi na minne pekee. “Baadhi ya miili bado mipya, mingine iko katika hali mbaya ya kuoza,” Richard Njoroge, mtaalamu wa uchunguzi katika kesi hiyo, aliwaambia waandishi wa habari juzi Ijumaa.

“Hakuna mtu aliyejitokeza kudai mpendwa wake”

Kulingana na uchunguzi wa awali wa miili, miili tisa ni ya vijusi vilivyozaliwa kabla ya wakati, kumi ni watoto wachanga waliozaliwa mfu, na wanane ni watu wazima, wanne kati yao wana majeraha vichwani. Vipimo vya DNA vitafanywa katika siku zijazo ili kubaini utambulisho wa miili hiyo. “Hakuna mtu aliyejitokeza kudai mpendwa wake. Na hatujapokea ripoti zozote za watu waliopotea pia,” anasema Martim Mwenda, afisa wa polisi huko Kericho.

Eneo la tukio limepanuliwa

Wapelelezi walitangaza kuwa wamepanua wigo wa uchunguzi wao hadi Nyamira, kaunti jirani ya Kericho, ambapo wanapitia maombi ya vibali vya mazishi. Mwishoni mwa wiki  iliyopita, hospitali ya Nyamira ilithibitisha kwamba miili kumi na mitatu ambayo haijadaiwa imehamishwa kutoka chumba cha kuhifadhia maiti hadi Kericho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *