Shirika la Waandishi wa HabariWasio na Mipaka (RSF) limechapisha ripoti siku ya Alhamisi, Machi 26, kuhusu hali ya uandishi wa habari katika eneo la Maziwa Makuu. 

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uganda, Kenya, Tanzania… Katika nchi hizi zote, hali ni zinafanana: imekuwa vigumu na hatari zaidi kufanya kazi ya uandishi wa habari. Waandishi wa habari wamekamatwa na kupigwa wakati wa uchaguzi nchini Uganda na Tanzania, au kufungwa jela kwa habari zao zinazoonekana kuwa za kukosoa sana utawala, kama ilivyo nchini Rwanda na Burundi. Na mashariki mwa DRC bado ni mahali ambapo uandishi wa habari unalipa gharama kubwa zaidi katika vita.

Waandishi wa habari watano wameuawa, watano hawajulikani walipo, 155 wamekamatwa au kuchukuliwa mateka katika miaka mitano iliyopita… 

Mashariki mwa DRC bado ni kitovu cha vurugu dhidi ya waandishi wa habari katika eneo hilo, inasema RSF. Tangu kundi lenye silaha la AFC/M23 lilipoteka miji ya Goma na Bukavu mwaka mmoja uliopita, kuripoti huru kutoka eneo hilo kumekuwa karibu kutowezekana, anabainisha Jeanne Lagarde, mwandishi mwenza wa ripoti ya RSF. “Msemo unaojirudia ni kwamba waandishi wa habari wako katikati ya vitisho vya M23 na vikosi vya jeshi vya DRC. Tangu kuanguka kwa mji wa Goma kutoka mikonoi mwa jeshi la FARDC kweda mikononi mwa waasi wa M23, angalau waandishi wa habari wanane wamekamatwa kwa siku kadhaa katika ofisi za zamani za idara ya ujasusi (ANR), ambazo zinaitwa ‘Gereza la Mbwa mkali.’ Waandishi wa habari wengi pia wametishiwa. Hii ndiyo kesi ya Amisi Musada, mwandishi wa habari wa Debout RDC, ambaye alitekwa nyara Aprili 15 mwaka jana na kupatikana siku chache baadaye katika hali ya kutatanisha.”

“Hii ni sera iliyopangwa vizuri ya kudhibiti masimulizi yanayowasilishwa na vyombo vya habari.” Vituo vya redio vya kijamii viko mstari wa mbele, inabainisha RSF, vimeporwa na kuharibiwa. Thelathini na tatu kati ya redio hizo zimeamriwa kufunga matangazo yao katika mwaka mmoja, mara nyingi kwa kukataa kutekeleza kufanya kazi kwa niaba ya mamlaka au makundi yenye silaha, anashuhudia mwandishi huyu wa zamani wa habari kutoka Goma, ambaye hakutaka jina litajwe. “Kwa mfano, kulikuwa na mitihani ya kumaliza shule ya msingi kwa wanafunzi na mitihani ya serikali, ambayo ilikuwa ikisimamiwa na serikali ya Kinshasa. Waasi walisema kwamba hili halipaswi kutajwa. Walisema kwamba kutokana na utawala wao mzuri, wanafunzi walikuwa wakipata elimu. Hii ni sera iliyopangwa vizuri ya kudhibiti masimulizi yanayowasilishwa na vyombo vya habari.”

Vyombo vya habari vinalengwa kila mara

Kulingana na mwandishi huyu, karibu wenzake hamsini wameondoka katika eneo hilo katika mwaka mmoja. Huko kaskazini, mkoa wa Ituri unaenelea kuwa moja ya maeneo hatari zaidi nchini kwa waandishi wa habari, inabainisha RSF. Kwa kuongezeka kwa makundi yenye silaha katika mkoa huo, vyombo vya habari vinalengwa kila mara, analalamika mwandishi huyu wa habari kutoka Bunia, ambaye pia anapendelea kutotajwa jina kwa sababu za kiusalama. “Kuna vita kila mahali katika mkoa wa Ituri. Na kwa hivyo, sisi ni kama tunalengwa kwa sababu tuko katikati. Upande mmoja, kuna serikali, kwa upande mwingine, pande zinazopigana. Ukiripoti shambulio dhidi ya jamii nyingine, zingine zinakuona mara moja kama adui.”

Ukatili unaohusishwa na mzozo huo, lakini pia vurugu za kisiasa. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, RSF imerekodi kukamatwa kwa waandishi wa habari zaidi ya 250 nchini, anaelezea Jeanne Lagarde. “Mikoa mingi imeathiriwa, kwa waandishi wa habari kuhukumiwa, kukamatwa, na kuwekwa kizuizini, mara nyingi hufanywa na magavana wa mikoa. Mfano mmoja ni kuzuiliwa kwa muda mrefu kwa Stanis Bujakera Tshiamala, aliyekamatwa mnamo mwezi Septemba 2023 na kushikiliwa kwa miezi sita.”

Ukatili huu unaoongezeka unazidishwa na ugumu wa kiuchumi na mfumo wa kisheria wenye vikwazo zaidi. Hivi ni baadhi tu ya vikwazo vinavyowakabili waandishi wa habari wa Kongo, ambao wanalazimika kuamua kuachana na habari wanaztaka kufanya, linahitimisha shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka, RSF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *