Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Andrea Mathew, amesema Serikali inatarajia kuanza kwa awamu ujenzi wa majengo ya Chuo cha Maji katika Kampasi ya Singida kuanzia mwaka wa fedha 2026/27.

Hatua hiyo inalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ufanisi katika utoaji wa mafunzo kwa wanafunzi wa kada ya maji na sekta zinazohusiana.

Akijibu swali la Mbunge wa Singida Mjini, Mheshimiwa Yagi Maulid Kiaratu, Kundo ameeleza kuwa Chuo cha Maji ni wakala wa Serikali ulio chini ya Wizara ya Maji ulioanzishwa mwaka 1974 kwa lengo la kuzalisha wataalam wa sekta ya maji pamoja na maeneo mengine kama umwagiliaji na ujenzi.

Ameongeza kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu katika ngazi ya stashahada, shahada na uzamili.

Mhandisi Mathew amefafanua kuwa kwa sasa Makao Makuu ya Chuo cha Maji yapo Dar es Salaam yakitumia majengo ya Ubungo kwa shughuli za kitaaluma, huku Kampasi ya Singida ikiendesha mafunzo katika majengo ya Bodi ya Maji ya Bonde la Kati. Alisema hali hiyo imekuwa na changamoto ya miundombinu isiyotosheleza mahitaji ya sasa.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *