Matukio ya ndege za kivita za Marekani kuangushwa huwa hayatokea mara kwa mara, hatua ya ndege hizo kudunguliwa nchini Iran ikiibua mjadala kuhusu mwelekeo wa vita mashariki ya kati.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ndege tatu za kivita za Marekani aina ya F-15 ziliangushwa nchini Kuwait mapema mwezi Machi katika kile Marekani ilisema lilikuwa tukio ambalo halikukusudiwa.

Wahudumu wote sita waliokuwa kwenye ndege hizo waliripotiwa kuokolewa.

Wahudumu wengine sita waliripotiwa kuuawa katika tukio jengine la ndege za kujaza mafuta za Marekani Machi 12 Magharibi mwa Iraq.

Ndege ya kivita ya Marekani aina ya F-15
Ndege ya kivita ya Marekani aina ya F-15 via REUTERS – US AIR FORCE

Aprili  7 2003,  ndege ya kivita ya Marekani aina ya F-15E iliangushwa katika oparesheni nchini Iraqi na kusababisha kifo cha rubani wake kwa jina la  Eric Das na afisa wa silaha William Watkins.

Kulingana na ripoti ya Marekani, ndege hiyo iliondoka katika kambi ya wanajeshi wa angani ya Al Udeid nchini Qatar kuelekea kwenye oparesheni maalum karibu na eneo la Tikrit, Iraq.

Aidha ndege nyengine ya kivita ya Marekani aina na A-10 iliaminika kuangushwa na kombora jijini Baghdad, Iraq, Aprili 8 2003, kulingana na taarifa ya jeshi la anga la Marekani.

Mabaki ay ndege ya kivita ya Marekani ambayo Iran imesema iliangusha.
Mabaki ay ndege ya kivita ya Marekani ambayo Iran imesema iliangusha. via REUTERS – IRIB

Rubani aliripotiwa kuokolewa kabla ya ndege hiyo kuanguka.  

Ndege nyengine ya kivita aina ya F-15E ilianguka kaskazini Mashariki mwa Libya mwezi Machi mwaka wa 2011.

Ndege nne na helikopta mbili zilitumwa kumtafuta rubani wa ndege hiyo ya F-15E kwa mujibu wa ripoti ya jeshi la Marekani wakati huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *