Wakulima wa parachichi wa kijiji cha Ilolo kata ya Kiwila wilaya ya Rungwe wameazimia kuunda kamati zitakazowapokea wanunuzi na kuwatambukisha kwa wakulima ili kuhakikisha wanafanya biashara na wanunuzi na mawakala waliosajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA).

Maazimio hayo yamefikiwa baada ya wataalamu wa COPRA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kukutana na wakulima hao na kuwapa elimu ya kufanya biashara na wanunuzi wanaotambulika ili kuepuka ununuzi holela unaopelekea kudhulumiwa na kuibiwa mazao yao.

Mkuu wa COPRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Samwel Msuya amewapengeza wakulima hao kwa kuunda kamati hizo na kuwasisitiza kuanza jitihada za kuunda vyama vya ushirika ili wafanye biashara kwa umoja kwa kuzingatia maslahi yao.

Amewafafanulia kuwa endapo watakuwa na ushirika imara watafanya biashara kwa haki na uwazi nq wataweza kukopesheka na taasisi za kifedha na hatimaye wataepuka unyonyaji wanaofanyiwa na baadhi ya wafanyabiashara na madalali.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *