Hivi  leo raia wa Rwanda na dunia kwa ujumla wanakumbuka kuanza kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, ambapo watu zaidi ya laki 8 wengi wao Watusi waliuawa ndani ya siku 100.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

April 7 ni moja ya siku muhimu katika historia ya Rwanda, taifa ambalo miaka 32 iliyopita lilipitia moja ya sura zenye giza zaidi katika historia ya mwanadamu.

Katika siku hii, kufuatia mauaji ya aliyekuwa rais wa taifa hilo, Juvenal Habyarimana, vurugu zilizuka nchi nzima na kilichofuatia ni mauaji ya kimbari kati ya Wahutu na Watusi, tukio ambalo watu zaidi ya milioni moja wanaripotiwa waliuawa katika siku 100 zilizofuata.

Wanaume, wanawake na watoto walilengwa katika mashambulio ya kupangwa, jamii zikiparaganyika, na kwa mwezi mmoja jumuiya ya kimataifa ilitazama kilichotokea bila kuchukua hatua kuzuia mauaji hayo.

Katika siku hii, raia wa Rwanda wanasimama kukumbuka na kutafakari kilichotokea, siku hii ikipewa jina KWIBUKA kwa maana ya ‘tunakumbuka’, benderea zikipepea nusu mlingoti huku rais Paul Kagame akitarajiwa kuwasha mwenge katika makavazi ya Kigali.

Licha ya kilichotokea, katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita, taifa la Rwanda limeshuhudia mabadiliko makubwa, kutoka katika jamii iliyokuwa imegawanyika na kuwa wamoja, hatua kubwa za maendeleo ya kijamii na kiuchumi zikipigwa, maridhiano yakipewa kipaumbele na haki ikiendelea kupatikana kwa wahanga wa vitendo vya mauaji ya kimbari.

Leo hii Rwanda inasimama kama taifa la mfano kwa Dunia, wito wa kutorejelewa tena kwa mauaji yaliyoshuhudiwa Rwanda ukitolewa na kusisitizwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *