Tukio limefanyika kata ya Buhanda, Manispaa ya Kigoma Ujiji, mkoani Kigoma, Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania, wananchi wanapata maelezo kuhusu lishe bora na matumizi sahihi ya vyakula vinavyozalishwa katika maeneo yao.

Fahamu mafungu sita ya chakula

FAO inataja mafungu sita chakula kwenye mlo kuwa ni mosi Nafaka, mizizi na ndizi mbichi; pili Mboga; tatu matunda; nne mafuta salama,; tano, vyakula vya asili ya wanyama na ndege; sita vyakula vya jamii ya mikunde, mbegu za mafunta na jamii ya karanga.

Wanawake wawili wa Kiafrika katika maeneo ya vijijini Tanzania wakitayarisha mboga za hali ya juu nje. Mwanamke mmoja anaketi kwenye nyasi akigandisha karoti, wakati mwingine anapiga magoti karibu na kikapu. Picha hiyo inaonyesha maandalizi ya chakula na lishe katika mazingira ya kilimo.

FAO yapatia wakazi wa Kigoma nchini Tanzania mafunzo ya vitendo kuhusu lishe bora

Wananchi walioneshwa mazao yaliyoongezewa virutubisho kama vile viazi lishe vyenye rangi ya chungwa, mahindi lishe na alizeti.

Wananchi pia wamepika uji unaoongezewa virutubisho kwa kutumia mahindi lishe yanayolimwa eneo lao. Uji huu unafaa kwa wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Mapishi ya uji wa mahindi  ya lishe

Salome John akionekana akikwangua karoti anasema kwenye  uji wa mahindi ya lishe wanaweka karoti, pilipili hoho, sukari, mafuta na rojo la karanga au mnoge. 

Mshauri wa kilimo mkoa wa Kigoma, James Peter anasema, “kuna makundi zaidi ya sita ambayo yanatakiwa kuchanganywa kwenye mlo mmoja. Sasa kutokana na nafasi na majukumu waliyonayo wakina mama zetu wakati mwingine wanaona uvivu kuyaandaa. Sasa kuna mazao ambayo yameshaandaliwa na kufanyiwa utafiti kwamba yameongezwa virutubisho kibaiolojia ambayo yanaweza kupunguza ule muda au kuondolea uvivu akina mama katika kuandaa kwa sababu tayari yana vitu vingi ambavyo vinaweza vikawa vimebeba karibu makundi mawili au matatu ya yale sita ambayo ni muhimu.”

Naye Edwin Katula, Afisa Kilimo wa Manispaa ya Kigoma Ujiji akatoa shukrani zake kwa FAO kwa kuwapatia mafunzo kwa vitendo pamoja na kuandaa tukio zima.

Lishe ndio msingi kama anavyosema Afisa Lishe wa Mtaa Happiness Adam kwamba ni vema kuhakikisha mafungu sita ya chakula kwenye mlo mmoja. Hata hivyo anasema, “tunashukuru akina mama wamefika na wamejifunza. Tunaomba na akina baba wajitokeze kwenye matukio kama haya kwani suala la lishe kwa mtoto ni la baba na mama.”

Pamoja na kilimo na lishe, huduma za chanjo zilipatikana kwa watoto na wanajamii waliohudhuria. Muuguzi Bernadetta Ukasi amesema chanjo walizotoa ni dhidi ya polio, pepopunda, dondakuu, surura na kuzuia kuhara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *