Mwanamke mmoja mwenye ushawishi mkubwa mitandaoni mwenye umri wa miaka 31 kutoka Miami nchini Marekani, alipatikana amekufa kwenye hoteli ya kifahari huko nchini Zanzibar katika mazingira ya kutatanisha, na familia yake inatafuta majibu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ashly Robinson, anayejulikana zaidi mtandaoni kama Ashlee Jenae, alipatikana amepoteza fahamu chumbani kwake katika hoteli moja nchini Zanzibar. Alipelekwa katika kituo cha matibabu kilicho karibu, ambapo alitangazwa kuwa amefariki dunia saa kadhaa baada ya kulazwa.

Uchunguzi wa kina kuhusu kifo cha kushutsha cha Robinson tayari unaendelea, kulingana na jamaa zake.

Ashly Robinson alisafiri hadi Zanzibar kusherehekea siku yake ya kuzaliwa Aprili 5. Wakati wa safari yake, mchumba wake, Joe McCann, alimpa Zawadi ya kushtukiwa kwa kumvisha pete ya ndoa wakati wa safari. Tukio hilo lilielezewa na familia ya Robinson kama la kukumbukwa. Wanandoa hao walikaa kwenye hoteli ya kifahari Zanzibar, wakati Ashly alipougua.

Familia za Robinson na Endres zilisema kwamba zinasaidia mamlaka za Zanzibar katika uchunguzi unaoendelea, lakini ziliwaomba kila mtu kuzingatia taarifa zote, isipokuwa zile zinazotoka kwa familia, kama zisizoaminika. Polisi nchini visiwani ikisema inasubiri uchunguzi wa upasuaji.

Hakuna taarifa kwa umma zilizotolewa na Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *