Viongozi wa Israeli na Lebanon watafanya mazungumzo siku ya Alhamisi, Aprili 16, Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza siku ya Jumatano jioni, siku moja baada ya mazungumzo ya kwanza ya moja kwa moja kati ya nchi hizo mbili.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Tunajaribu kuweka utulivu kidogo kati ya Israel na Lebanon. Imekuwa muda mrefu tangu viongozi hao wawili wazungumze, takriban miaka 34. Viongozi hao watazungumza. Vizuri sana!” Donald Trump aliandika kwenye mtandao wake wa Truth Social.

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa alaani ” matukio ya kikatili yanayotokea ndani ya makazi ya watu” Lebanon 

Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki ya Makazi amejiunga na wataalamu wengine wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa katika kuihimiza Israel kukomesha mara moja kampeni yake ya mashambulizi nchini Lebanon.

Balakrishnan Rajagopal ameandika kwenye mitandao ya kijamii kwamba jeshi la Israel lilikuwa likitumia “mkakati uleule” kusini mwa Lebanon kama ilivyo Gaza au Ukingo wa Magharibi unaokaliwa. Hii inajumuisha ” mauaji ya kikatili yanayotokea ndani ya makazi ya watu na kuwahamisha raia kwa nguvu… unyakuzi wa ardhi kupitia ‘maeneo yasiyokuwa na jeshi’ na walowezi kunyakua ardhi zisizokuwa  zao,” Rajagopal ameandika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *