Mbunge wa Vitı Maalumu Mkoa wa Arusha, Mhe. Martha Gido amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mapinduzi na hatua kubwa za maendeleo zilizopigwa Mkoani Arusha katika kipindi chake cha uongozi, akisema hatua hiyo imechochea ustawi na maendeleo ya Mkoa wa Arusha hasa kwa wanawake wa Mijini na Vijijini. Mhe. Gido amebainisha hayo leo Jumatano Aprili 22, 2026 Bungeni Mjini Dodoma wakati akichangia kwenye mjadala wa Bajeti ya Wizara ya nishati kwa mwaka 2026/27, akitaja hatua hizo za maendeleo kuwa ni pamoja na usambazaji mkubwa wa huduma za umeme ambazo zimefika katika Vijiji na Vitonaoii vindi vva Mkoa wa Arusha.Mbunge huyo amesema kutekelezwa kwa mradi wa kuzalisha umeme wa Bwawa la Julius Nyerere Mkoani Pwani pamoja na kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera ni miongoni mwa miradi mikubwa iliyotekelezwa na serikali ya awamu ya sita, akibainisha kuwa mafanikio yake ni pamoja na kusisimua uchumi, kutokomeza tatizo la mgao wa umeme pamoja na kupunguza gharama za uzalishaji kwa kuwatenga wananchi na wafanyabiashara dhidi ya matumizi ya majenereta.
Katika mchango wake Mhe. Gido kando pia ya kumpongeza Waziri wa nishati Mhe. Deogratius Ndejembi na wasaidizi wake kwa kutekeleza kwa vitendo maono ya Rais Samia, akiomba serikali kuharakisha.
(Feed generated with FetchRSS)