KIUNGO mshambuliaji ENPPI, Arafat Masoud ‘Kondeboy’, amesema ameanza kuelewa ushindani wa soka la Misri baada ya kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu na anahitaji kupambana zaidi ili kupata nafasi ya kudumu kikosini.

Konde Boy, ambaye ni zao la Azam FC, amesema tangu mzunguko wa pili wa ligi hiyo ameshuhudia ushindani mkubwa wa nafasi na hata ligi hiyo.

“Kuanzia nafasi ya kwanza hadi ya saba tayari tumecheza mechi zetu sita za mzunguko wa pili, kuanzia nafasi ya nane hadi ya 21 wao wanaendelea na ratiba yao. Ushindani ni mkubwa na siyo rahisi kupata nafasi,” amesema Konde Boy na kuongeza; alipata dakika chache za kucheza katika baadhi ya mechi, jambo lililompa uzoefu mwingine kuhusu soka la nchi hiyo.

KOND 01

“Nilipata nafasi kidogo kwenye mechi za kombe la ndani, nimejifunza mengi na ninaona bado nahitaji kupambana zaidi msimu ujao. Ligi ya huku ni ngumu sana, si rahisi kama watu wanavyofikiria,” alieleza.

Konde Boy amesema anaamioni msimu ujao atakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kufanya vizuri na kupigania nafasi ya kucheza mara kwa mara.

ENNPI iko nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi na pointi 30 kwenye mechi 20, imeshinda saba, sare tisa na kupoteza nne.

KOND 02

Kiungo huyo alitambulishwa ENPPI akitokea Fountain Gate FC alikokuwa kwa mkopo akitokea Azam FC na alicheza mechi nne dhidi ya Coastal Union, Tanzania Prisons pamoja na Stand United katika hatua za mtoano (playoff).

Kabla ya hapo, alijiunga na Azam FC mwaka 2017 akianzia timu za vijana za U-17 na U-20 kabla ya kupandishwa kikosi cha wakubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *