Serikali imeendelea kupiga hatua kubwa katika kulinda na kuimarisha haki za binadamu, hatua ambazo zimechangia kudumisha amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa huku wadau wa sekta ya sheria wakitakiwa kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi, zenye ushahidi na takwimu thabiti ili kuimarisha uwazi na uaminifu wa taarifa zinazowasilishwa kitaifa na kimataifa.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainabu Katimba, Mkoani Morogoro wakati wa kikao kazi cha kupitia na kuhakiki rasimu ya taarifa ya hali ya haki za binadamu nchini ili kuwasilisha taarifa hiyo katika Umoja wa Mataifa na kusisitiza umuhimu wa kutoa taarifa sahihi na zenye takwimu

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Richard Kilanga, ameeleza kuwa kikao hicho kina lengo la kuimarisha ubora wa taarifa pamoja na kuweka msingi imara wa utekelezaji wa majukumu ya kulinda haki za binadamu.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *