#HABARI:Mwalimu Geofrey Pascal Paul wa Shule ya Sekondari Hai mkoani Kilimanjaro ameibuka mshindi wa gari aina ya Mazda CX5 kupitia kampeni ya “Mwaka Umenyooka” inayoratibiwa na My Airtel App, na hivyo kubadilisha kwa kiasi kikubwa maisha yake ya kila siku.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa gari hilo iliyoandaliwa na Airtel Tanzania, Mwalimu Paul alisema ushindi huo ni hatua kubwa kwake, hasa katika kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake ya kikazi. Alieleza kuwa awali alikuwa akitegemea usafiri wa pikipiki kwenda na kurudi shule, hali iliyokuwa ikimpa changamoto hasa nyakati za mvua, lakini sasa ana uhakika wa usafiri salama na wa uhakika zaidi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Airtel Money wa Airtel Tanzania, Andrew Rugamba, alisema kampeni hiyo inalenga kurudisha kwa jamii pamoja na kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidigitali. Aliongeza kuwa kupitia Airtel Money App, Watanzania wanaweza kufanya miamala mbalimbali kwa urahisi zaidi huku wakichangia kukuza uchumi wa kidigitali nchini.
(Feed generated with FetchRSS)