Katika taarifa iliyotolewa katika mji mkuu wa Denmark, Copenhagen tarehe 4 Mei 2026, Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Ulaya, Dkt. Hans Henri P. Kluge, amesema shirika hilo linafanya kazi kwa haraka kusaidia juhudi za kukabiliana na tukio hilo, ikiwa ni pamoja na huduma za matibabu, uokoaji wa wagonjwa, uchunguzi na tathmini ya hatari kwa afya ya umma.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa WHO Ulaya inaendelea kushirikiana na nchi husika ili kuhakikisha hatua zilizoratibiwa na zinaozingatia sayansi. Dkt. Kluge amezishukuru mamlaka za Afrika Kusini kwa msaada wao wa haraka, ikiwemo kumhudumia mgonjwa kutoka Uingereza.

Ameeleza kuwa maambukizi ya Hantavirus si ya kawaida na mara nyingi huhusishwa na  panya walioambukizwa mardahi hayo. Ingawa yanaweza kuwa makali katika baadhi ya maambukizi, hayasambai kirahisi kutoka mtu hadi mtu.

“Hatari kwa umma kwa ujumla bado ni ndogo. Hakuna haja ya taharuki au vikwazo vya usafiri,” amesisitiza.

Dkt. Kluge ameongeza kuwa tukio hilo ni ukumbusho muhimu kwamba vitisho vya afya haviheshimu mipaka ya nchi, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kulinda maisha ya watu.

Unaweza kusoma zaidi hapa kuhusu ugonjwa huu hapa

Hali ikoje Afrika?

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika limesema linafuatilia kwa karibu na kutoa msaada unaohitajika tukio la afya ya umma kuhusu ugonjwa wa Virusi vya Hanta uliothibitishwa kutokea katika meli ya kitalii iliyosafiri katika Bahari ya Atlantic ambapo mpaka kufikia sasa watu watatu wamepoteza maisha. 

Akitoa taarifa hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa X, Mkuu wa WHO Kanda ya Afrika Prof. Mohamed Janabi amesema hadi kufikia jana tarehe 3 Mei, Mgonjwa mmoja aliyekuwa na maambukizi ya kirusi cha Hanta au hantavirus alimethibitishwa maabara, huku wengine watano wakiendelea kufanyiwa uchunguzi. 

Akieleza hali ikoje barani la Afrika Profesa Janabi amesema “Kwa Afrika, hatari bado iko chini kwa wakati huu, lakini umakini wetu uko juu. Tunaimarisha ufuatiliaji na maandalizi ili kuhakikisha tunashughulikia kwa uharaka na ufanisi.”

Amewatoa hofu wananchi kwa kusema kuwa “Acha niwahakikishie umma kwamba hili ni tukio zito lakini limedhibitiwa na hakuna haja ya hofu au vikwazo vya usafiri katika hatua hii. Lengo letu liko wazi: kuokoa maisha, kudhibiti hatari na kuhakikisha kwamba nchi zinaungwa mkono kikamilifu na hatua zinazotegemea sayansi.

Kwa sasa WHO inafanya kazi kwa karibu na nchi husika na waendeshaji wa meli hiyo ili kusaidia huduma za matibabu, kuratibu uokoaji na kufanya tathmini kamili ya hatari ya afya ya umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *