
Iran inasema makombora yake mawili yamelenga meli ya kivita ya Marekani kwenye mlango wa Bahari ya Hormuz, baada ya nchi hiyo kupuuza onyo lake la kutopita katika eneo hilo, ambapo pia Marekani inazuia meli za Iran.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Vyombo vya Habari nchini Iran, vimewanukuu wako wa jeshi la Iran, ambao wamesema shambulizi hilo linaonesha kuwa mlango wa Bahari wa Hormuz umefungwa, na ni onyo kwa Marekani.
Hata hivyo, jeshi la Marekani limekanusha madai hayo ya Iran, ikisema hakuna meli yake iliyoshambuliwa na zimepita kwa usalama katika eneo la mlango wa Bahari ya Hormuz.
Hii inakuja baada ya rais Donald Trump, kutangaza kuwa wanajeshi wa Marekani, wataanza kusaidia kupunguza foleni ya meli zaidi ya Elfu mbili za mizigo, zilizokwama katika eneo hilo la Bahari tangu kuanza kwa vita mwezi Februari.
Wachambuzi wa masuala ya mizozo wanaonya kuwa, iwapo meli za Marekani zililengwa na jeshi la Iran, basi ni kiashiria kuwa huenda vita vikarejelewa tena na hivyo makubaliano ya usitishwahi vita yaliyfanyika wiki nne zilizopita ili kupisha mazungumzo ya amani, yakavunjika.
Katika hatua nyingine, nchi ya Falme za Kiarabu imesema meli yake ya mafuta imeshambuliwa katika mlango wa Bahari wa Hormuz.