Nchini Madagascar, maadhimisho ya Wiki ya Ulaya, ambayo yanaanza Mei 5, yanatoa fursa kwa Umoja wa Ulaya kukumbusha jukumu lake katika kisiwa hiki na hadhi yake kama mfadhili mkubwa zaidi wa nchi hii. Katika muktadha mgumu hasa—kukamatwa kwa vijana, wanaharakati wa vuguvugu la Gen Z na kua na uhusianow na Moscow kuhusu uchaguzi—balozi wa Umoja wa Ulaya ametetea jukumu la washirika wa kidemokrasia na kutoa wito wa kuheshimiwa kwa utawala wa sheria.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Antananarivo, Sarah Tétaud

Madagascar inaendelea na uhusiano na Urusi. Katikati ya mwezi Aprili, rais wa Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi nchini Madagascar (CENI) alisafiri hadi Moscow kuchunguza ushirikiano katika uwasilishaji wa matokeo ya uchaguzi.

Hatua hii inayatia wasiwasi mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kiraia katika nchi ambayo majaribio ya kuingilia kati ya Urusi yalikuwa tayari yamerekodiwa wakati wa uchaguzi wa urais wa mwaka 2018.

Mbele ya waandishi wa habari, Balozi Roland Kobia alichagua mchakato wa kujenga uhusiano mwema kati ya mataifa kwa kuwalenga raia wa kawaida badala ya mzozo: “Madagascar ina haki ya kuchagua na kubadilisha washirika wake. Hata hivyo, lazima tukumbuke baadhi ya misingi: 90% ya misaada, uwekezaji, na biashara inayotolewa kwa Madagascar inatoka katika nchi za kidemokrasia (mataifa yanayofuata mfumo wa utawala ambapo wananchi wana mamlaka ya juu).”

“Siko hapa kushiriki katika shindano la urembo”

Hii ni njia ya kuonyesha uzito wa Umoja wa Ulaya (EU), mfadhili mkubwa zaidi wa nchi hiyo, tofauti na Urusi, ambayo anaielezea, bila kuitaja waziwazi, kama mfano mwingine: “Tunafanya kazi katika nyanja za afya, elimu, maendeleo ya vijijini, na sekta muhimu za kijamii. Ushirikiano wetu hauzuiliwi kwa sekta moja au mbili ambazo zinaweza kuwa kwa maslahi ya ujio wa hivi karibuni.” Kuhusu uchaguzi, siko hapa kushiriki katika shindano la urembo: Nadhani nchi za kidemokrasia labda zina utaalamu zaidi kuliko zingine katika kuhakikisha uchaguzi wa haki.

Suala jingine nyeti: kukamatwa kwa vijana kutoka vuguvugu la Gen Z, vuguvugu lililochangia Kanali Randrianirina kuingia madarakani mwishoni mwa 2025. Tangu mwezi Aprili, wanaharakati kadhaa wamekamatwa kwa “kuhatarisha usalama wa taifa” baada ya maandamano ya amani.

“Sisi pekee, pamoja na marafiki zetu wa wanaopenda demokrasia, tulikuwa tukitoa taarifa mbili za umma tukiwataka mamlaka wakati wa matukio (mwezi Septemba mwaka uliyopita) kuwalinda vijana na kuanzisha mazungumzo. Hatujasikia nchi nyingine nyingi zinazojadiliwa leo. Tunatumai kwamba suluhisho chanya litapatikana kwa vijana hawa wote ambao wamekamatwa au ambao bado wako kizuizini. Vijana wa Madagascar lazima wasikilizwe na sauti zao zizingatiwe,” amehitimisha Roland Kobia.

Onyo mchanganyiko, wakati ambapo Madagascar inaonekana kuwa inapita kati ya mifumo miwili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *