Uhaba wa makazi bora na yenye staha nchini umeendelea kuwa changamoto kubwa, huku ikielezwa kuwa Tanzania ina upungufu wa nyumba zaidi ya milioni tatu.
Aidha, mahitaji mapya ya nyumba yanakadiriwa kuongezeka kwa takribani nyumba laki tatu kila mwaka.
Mkurugenzi wa Taasisi ya TMRC, Elibariki Ndosi, amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa hati ya taarifa muhimu ambayo ni msingi wa utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Hati Fungani za Muda wa Kati wenye thamani ya hadi Shilingi bilioni 100.
Ndosi amesema hatua hiyo inalenga kusaidia upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya makazi, ili kupunguza changamoto ya uhaba wa nyumba bora na kuwezesha Watanzania wengi zaidi kumudu makazi yenye hadhi.
Mhariri | @rajjmsangi
#AzamTvUpdates
(Feed generated with FetchRSS)