Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limetoa cheti cha pongezi kwa chombo cha habari Channel Ten kwa kutambua mchango wake mkubwa katika mapambano dhidi ya uhalifu na kuimarisha usalama wa raia na mali. Kupitia ushirikiano wa karibu na wa kitaaluma uliodhihirishwa katika kuripoti habari na kuelimisha umma kuhusu masuala ya ulinzi na usalama, Channel Ten imewezesha Jeshi la Polisi kufikisha elimu muhimu kwa wananchi, jambo lililochangia kuimarika kwa miundombinu ya amani, ulinzi na usalama.

Jeshi hilo limeeleza kuwa mchango wa chombo hicho umekuwa na umuhimu mkubwa katika kuzuia, kutanzua na kukabiliana na vitendo vya uhalifu pamoja na wahalifu, na hivyo kusaidia kudumisha utulivu na ustawi wa jamii.

@deilahmomo

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *