Mkutano wa siku mbili kati ya Ufaransa na mataifa ya Afrika unaanza leo jijini Nairobi nchini Kenya.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unalenga kuangazia upya ushirikiano kati ya nchi ya Ufaransa na Mataifa ya Afrika kwenye nyanja mbalimbali.

Siku ya kwanza, mkutano huu unatarajiwa kuwakutanisha wafanyabiashara wa Ufaransa na wale kutoka barani Afrika, kuangazia maeneo muhimu ya uwekezaji.

Katika chuo kikuu cha Nairobi, rais William Ruto na Emmanuel Macron wanatarajiwa kukutana na vijana kujadili mausala mbalimbali ya fursa zilizopo kwenye ulimwengu wa teknolijia.

Siku ya Jumanne, kutakuwa na mkutano wa wakuu wa nchi mbalimbali kutoka Afrika na rais Macron, ambapo masuala mbalimbali yatajadiliwa  ikiwemo ushirikiano wa kiuchumi, siasa na usalama, ambapo mikataba kadhaa inatarajiwa kusainiwa.

Hii ndio mara ya kwanza, mkutano huu unafanyika katika nchi ambayo raia wake hawazungumzi Kifaransa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *