Kawaida kuanza ziara ya siku sita MtwaraKawaida kuanza ziara ya siku sita Mtwara

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Mohammed Ali  Kawaida anatarajia kuanza ziara ya siku sita mkoani Mtwara kuanzia Mei 18, 2026 kwa lengo la kukutana na vijana pamoja na wananchi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Ziara hiyo itamfikisha katika wilaya za Mtwara Mjini, Tandahimba, Newala, Masasi na Nanyumbu ambapo atapata nafasi ya kuzungumza na vijana kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo na ushiriki wao katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na UVCCM, ziara hiyo inalenga kuimarisha mawasiliano kati ya viongozi na vijana pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Wananchi na vijana wa Mkoa wa Mtwara wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mikutano na shughuli zitakazoandaliwa wakati wa ziara hiyo.

Aidha, UVCCM imewataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa kupitia kurasa zake rasmi pamoja na vyombo vya habari ili kupata ratiba na taarifa zaidi kuhusu ziara hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *