Bado safari ni ndefu kwa dunia kujiandaa ipasavyo dhidi ya milipuko ya magonjwaBado safari ni ndefu kwa dunia kujiandaa ipasavyo dhidi ya milipuko ya magonjwa

Akili mnemba au AI ina uwezo wa kuboresha maandalizi na kufuatilia vitisho vya milipuko ya magonjwa, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo huko Geneva, Uswisi na Bodi ya Kimataifa ya Kufuatilia Utayari wa dunia kukabili magonjwa, (GPMB).

Ingawa hivyo ripoti imesisitiza umuhimu wa usimamizi Madhubuti wa teknolojia hizo za kisasa ikionya kuwa “bila usimamizi madhubuti na hatua za ulinzi, ubunifu wa kiteknolojia unaweza kwa kweli kupunguza usalama wa afya na kuongeza pengo la upatikanaji wa huduma za afya lililoonekana wakati wa janga la coronavirus“>COVID-19.”

Ripoti hiyo ya kurasa 28 imetolewa leo wakati wa ufunguzi wa WHA ambao ni mkutano wa 79 wa Baraza la shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO.

Bodi hiyo ni chombo huru cha ufuatiliaji na uwajibikaji kilichoanzishwa na WHO mwaka 2018 pamoja na Benki ya Dunia — ikiwa ni wakala maalumu wa Umoja wa Mataifa — kwa lengo la kuimarisha maandalizi dhidi ya majanga ya afya duniani.

Bodi hiyo inaangazia kwamba uongozi wa kitaifa utakuwa kwenye mtihani mkubwa mwaka huu wakati serikali zinafanya kazi kukukamilisha Mkataba wa WHO wa Kukabili Majanga, (Pandemic Agreement), na kufikia makubaliano kuhusu “tamko la kisiasa la Umoja wa Mataifa” lenye maana kuhusu kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na milipuko ya magonjwa.

Ujumbe mkuu katika ripoti iyo umegawanywa katika maeneo makuu manne:

© WHO Kuwasili kwa msaada muhimu katika #Bunia ili kuimarisha majibu dhidi ya mlipuko wa Ebola huko Ituri.

Maandalizi ya kimataifa yanashindwa kwenda sambamba na hatari ya milipuko ya magonjwa.

  1. Ndani ya miezi michache baada ya ripoti ya kwanza ya GPMB kuonya kwamba dunia haikuwa tayari kwa janga linalosambaa kwa kasi, COVID-19 ilitokea, ikiwa janga hatari zaidi la magonjwa ya kupumua tangu mwaka 1918. Licha ya kuwepo kwa maarifa, zana na rasilimali nyingi zaidi, mwelekeo wa hatari ya milipuko ya magonjwa unaendelea kwenda upande usiofaa.
  2. Mabadiliko ya tabianchi na migogoro ya kivita vinaongeza hatari; mgawanyiko wa kisiasa wa kimataifa, kudhoofika kwa fursa za kiraia, na maslahi ya kibiashara binafsi vinadhoofisha hatua za pamoja. Uwezo mkubwa wa zana za hali ya juu za akili mnemba (AI) na teknolojia ya kidijitali kubadilisha maandalizi, kinga na mwitikio dhidi ya milipuko ya magonjwa (PPR) unadhoofishwa na — bila ulinzi na usimamizi madhubuti — unaweza kupunguza usalama wa afya na kuongeza pengo la upatikanaji wa huduma lililoonekana wakati wa COVID-19.

Ushahidi unatisha—imani imetoweka na ukosefu wa usawa ni dhahiri

Dharura za afya ya umma katika kipindi cha miaka 10 iliyopita—kuanzia Ebola hadi mpox—zinaonesha kwamba dunia haijawa salama zaidi dhidi ya athari zake mbaya, huku gharama za kiuchumi na kijamii zikiongezeka, upatikanaji wa hatua za kukabiliana na magonjwa ukizidi kudhoofika, ufadhili ukipungua, na jamii zikiibuka zikiwa maskini zaidi, zisizo sawa zaidi na zilizogawanyika zaidi. Maeneo muhimu yamepuuzwa, kuanzia mbinu ya Mfumo mmoja wa Afya na ushirikiano wa sekta mbalimbali hadi kuweka mizani sahihi ya hatua za afya ya umma na kijamii pamoja na kukabiliana na taarifa potofu.

Vipaumbele vya hatua za kuchukua

Imani ya kudumu na usawa endelevu kwa jamii vinaweza kuimarishwa, hata wakati wa kukabiliana na taarifa potofu, kwa kuanzisha:

  • ufuatiliaji huru, wa sekta mbalimbali na wa kina wa hatari za milipuko ya magonjwa, unaotumia teknolojia za kisasa kama AI lakini zinazozingatia maadili.
  • upatikanaji wa haki wa hatua za kukabiliana na magonjwa, kupitia kukamilishwa, kuridhiwa na utekelezaji kamili wa Mkataba wa WHO wa Kukabiliana na Majanga ya Magonjwa, pamoja na uwezo madhubuti wa uzalishaji wa kikanda, unaoungwa mkono na uhamishaji wa teknolojia, maendeleo ya nguvu kazi na uwekezaji unaolengwa;
  • ufadhili endelevu.

Umakini wa kisiasa

  • Maandalizi, kinga na mwitikio dhidi ya milipuko ya magonjwa (PPR) na hatari nyingine nyingi kwa zama za sasa havizuiliwi tena na uwezo pekee, bali pia na changamoto za hatua za pamoja ambazo zinaweza kutatuliwa na viongozi wa kisiasa pekee.
  • Ushiriki wa kisiasa wa kudumu na usioyumba ni muhimu sana, kuanzia na fursa mbili za kipekee mwaka 2026: kukamilisha Mkataba wa WHO wa Kukabiliana na Majanga ya Magonjwa, na kufikia makubaliano juu ya ahadi mpya na zenye maana katika Mkutano wa Pili wa Ngazi ya Juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu PPR ili kuendeleza ufuatiliaji huru, upatikanaji wa haki, na ufadhili endelevu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *