Wito umetolewa kwa Serikali kuongeza kasi ya kutatua migogoro ya ardhi ili kudumisha amani na kuimarisha imani ya wananchi kwa uongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wito huo umetolewa na Mbunge wa Kasulu vijijini Mhe. Edibily Kazala wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Mei 17, 2026 wilayani humo.
Edibily amesema wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini wanaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na hatua mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali katika maeneo yao.
Hata hivyo, amebainisha kuwa migogoro ya ardhi imeendelea kuwa changamoto inayohitaji ufumbuzi wa kudumu, akisisitiza kuwa utatuzi wake utasaidia kuimarisha mshikamano wa kijamii na kuharakisha maendeleo katika jimbo hilo.
(Feed generated with FetchRSS)
