Mbunge wa Mtwara Vijijini, Arif Suleiman Premji, ameishauri Serikali na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuhakikisha kunakuwa na usawa wa viwango vya riba vinavyotolewa na taasisi za kifedha kwa wananchi, akisema tofauti kubwa ya riba kati ya makundi mbalimbali inaendelea kuwa mzigo kwa wafanyabiashara na watumishi wa umma.
Akichangia mjadala bungeni, Premji amesema kwa sasa kiwango cha riba kuu cha BOT (CBR) ni asilimia 5.75, kiwango ambacho taasisi za kifedha hukopa, lakini wananchi wanaendelea kupata mikopo yenye riba kubwa isiyoendana na mazingira halisi ya uchumi.
Amesema wakulima wengi hupata mikopo ya riba ya asilimia 9 huku wafanyabiashara na watumishi wa umma wakikopa kwa riba inayofikia kati ya asilimia 14 hadi 20, hali aliyoieleza kuwa si ya haki.
Katika hatua nyingine, Premji ameishauri Serikali kuelekeza nguvu katika uwekezaji wa viwanda vya teknolojia, akisema Tanzania ina malighafi muhimu zinazotumika kutengeneza vifaa vya kisasa vya kielektroniki ikiwemo simu za mkononi.
(Feed generated with FetchRSS)
