MONUSCO yawezesha redio za Ituri kwa nishati ya jua na vifaa vya utangazajiMONUSCO yawezesha redio za Ituri kwa nishati ya jua na vifaa vya utangazaji

Vituo vilivyonufaika ni Radio Sauti Ya Injili (RSI), Radio Candip, Radio Tempête de Kasenyi (RTK), pamoja na Redio na Televisheni ya Taifa (RTNC). Kila kituo kilipokea paneli za sola, mifumo ya betri, kigeuza umeme na vifaa vya kinga dhidi ya radi ili kuhakikisha matangazo yanaendelea bila kukatizwa kutokana na ukosefu wa umeme.

Mkurugenzi wa Radio Candip, Freddy Lorima Dz’bo anasema, “msaada huu ni baraka kubwa. Tulikuwa tunategemea jenereta iliyokuwa ikitumia hadi lita 20 za mafuta kwa siku. Tangu kufungwa kwa paneli za sola, matangazo yetu yamekuwa endelevu.”

©MONUSCO Nishati ya Jua inawekwa katika vituo vya redio huko Ituri DRC. Vituo vya redio vya ndani vina jukumu muhimu katika kusambaza habari za kuaminika na kuongeza ufahamu miongoni mwa watu, mara nyingi katika lugha kadhaa za kienyeji.

Mradi huo pia unasaidia kampeni za uhamasishaji kuhusu Ebola kupitia matangazo ya lugha za wenyeji. Freddy Lorima anaongeza akisema,“sasa tunaweza kuandaa na kurusha vipindi siku nzima, ikiwa ni pamoja na ujumbe wa uhamasishaji kuhusu Ebola kwa lugha za wenyeji.”

Aidha, waandishi wa habari walipatiwa mafunzo ya uhakiki wa taarifa na maadili ya uandishi wa habari ili kukabiliana na habari za uongo. Mkurugenzi wa RTNC Ituri, Benx Mubengwa Katondji anasema, “sasa tuna uwezo mzuri zaidi wa kuhabarisha wananchi kuhusu masuala muhimu kama Ebola na kupambana na taarifa za uongo.”

Kwa mujibu wa MONUSCO, katika kipindi cha miaka minne iliyopita ujumbe huo umefadhili vituo 14 vya redio za kijamii katika maeneo mbalimbali ya Ituri kwa uwekezaji wa jumla wa dola 150,000 za Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *