Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, MheNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, ametoa mchango wa shilingi milioni 21 kwa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya kusaidia utoaji wa zawadi na uendeshaji wa shughuli za michezo, ikiwa ni hatua ya kuondoa changamoto ya ukosefu wa zawadi iliyokuwa ikiathiri mashindano mbalimbali ya mpira wa miguu kwa takribani miaka mitatu mkoani humo.

Mchango huo ameukabidhi kwa viongozi wa michezo mkoani humo wakati wa kuhitimisha mchezo wa fainali wa soka uliowakutanisha timu ya Kitope na Mundu, ambapo timu ya Kitope iliibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Mundu katika mchezo uliovutia mashabiki wengi.

Aidha, Naibu Waziri amesema fedha hizo zitatumika kufanikisha utoaji wa zawadi kwa timu zilizoshiriki mashindano ya misimu iliyopita pamoja na msimu wa sasa, hatua inayolenga kurejesha hamasa ya michezo kwa vijana na kuimarisha maendeleo ya soka katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kadhalika, Mhe. Ayoub amebainisha kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa michezo katika kujenga afya, kukuza uchumi na kuimarisha mshikamano wa jamii, huku akisisitiza umuhimu wa vijana kutumia michezo kama nyenzo ya kujiletea maendeleo badala ya kujihusisha na vitendo vinavyoweza kuharibu maisha yao.

#kilichoborakabisa

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *