Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na majukumu yake ya msingi ya kuzuia vitendo vya kihalifu na kwa ujumla h…Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na majukumu yake ya msingi ya kuzuia vitendo vya kihalifu na kwa ujumla h…

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na majukumu yake ya msingi ya kuzuia vitendo vya kihalifu na kwa ujumla hali ya Jiji ni salama.Hata hivyo tarehe 14 Mei, 2026 majira ya saa 04 :30 usiku Polisi walipokea taarifa kuwa katika majengo pacha ya ‘PSSSF’ Mtaa wa Mission Ilala Dar es Salaam watu wawili 1. Weiyi Chen miaka 64, mfanyabiashara, raia wa China na 2. Liang Xiolo miaka 44, mfanyabisahara raia wa China ilidaiwa walivamiwa na kutekwa na kundi la wahalifu waliodaiwa kuwa saba nakupelekwa kusiko julikana.

Polisi kwa kushirikiana na kamisheni zingine za uchunguzi za Jeshi hilo ilifanikiwa kupata namba za magari ambayo yalidaiwa kutumika katika tukiohilo. Gari moja wapo lililokamatwa baadae lilikutwa likiwa na namba T.305 DRP aina ya Toyota Alphard ambazo sio namba halisi za gari hilo na gari lingine lililokamatwa ni lenye namba T.188 DHT aina ya Toyota Harrier.

Watuhumiwa hao kabla ya kukamatwa walitoa vitisho kwa ndugu kuwa wapewe kwa njia ambazo wangewaelekeza dolla za kimarekani milioni 20 ili wawaachie.

Upelelezi wa Jeshi la Polisi ulifanikiwa kuwaokoa wahanga hao tarehe 16 Mei, 2026 na kukutwa wakiwa wamejeruhiwa na kuumizwa kwenye maeneo ya miili yao huko maeneo ya Mbezi Kinondoni.Wahanga walipelekwa hospitali ya Agakhan lakini Weiyi Chen bado hali yake sio nzuri na amelazwa katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es Salaam. Watuhumiwa 04 wamekamatwa baada ya ufuatiliaji mkali kufanyika kuhusiana na tukio hilo ambao ni ; 1. Deng Anqing miaka 49, raia wa China 2. Fan Zhong miaka 49, raia wa China 3. Zhang Jianjun miaka 51, raia wa China 4. Deng Qiang miaka 40, raia wa China. Wamekutwa na simu za wahanga na vielelezo vingine.

Upelelezi wa tukio hili unakamilishwa na kila aliyehusika katika tukio hili kwa namna moja ama nyingine atashughulikiwa vikali na kwa hatua stahiki zilizo ndani ya mfumo wa sheria. Polisi Dar es Salaam haikubaliani na vitendo vyovyote vya kihalifu na inaendelea kuwashukuru wananchi ambao wamekuwa wakitoa taarifa za kweli ambazo zimesaidia kuzuia uhalifu na zingine kuwakamata wanaojihiusisha na vitendo vya kihalifu

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *