Ebola nchini DRC: Mambo yanayofanya mlipuko wa Ebola kuwa mgumu zaidi kuudhibitiEbola nchini DRC: Mambo yanayofanya mlipuko wa Ebola kuwa mgumu zaidi kuudhibiti

Wakati wa mkutano wa mawaziri mtandaoni ulioandaliwa na Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magaonjwa cha Afrika (Africa CDC) siku ya Jumatatu, Mei 25, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus alizungumzia mambo makuu yanayofanya juhudi za kudhibiti mlipuko huu mpya wa Ebola nchini DRC kuwa mgumu.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesu alitaja mambo matatu: kugunduliwa kwa ugonjwa huo kwa kuchelewa, ukosefu wa usalama katika mikoa ya Kongo ya Ituri na Kivu Kaskazini, na kutoaminiana miongoni mwa wakazi wa eneo hilo, jambo ambalo limesababisha matukio mbalimbali.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inakabiliwa na mlipuko wa Ebola “mbaya na mgumu sana,” alionya mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Ghebreyesus siku ya Jumatatu, Mei 25, akitoa wito kwa nchi jirani kuchukua hatua “mara moja.”

Akizungumza katika mkutano wa mawaziri mtandaoni ulioandaliwa na Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC), pia alibainisha kwamba mambo kadhaa yanayofanya juhudi za kudhibiti mlipuko huu mpya wa Ebola nchini DRC kuwa mgumu.

Jambo la kwanza, ni kutambuliwa kwa kuchelewa kwa ugonjwa huo, akiongeza kwamba timu zinazopambana na virusi sasa zinajaribu kukabiliana na mlipuko huo. “Tunaongeza shughuli haraka, lakini kwa sasa, mlipuko unaendelea kwa kasi zaidi kuliko sisi,” alisema, kabla ya kuzungumzia jambo la pili: “ukosefu wa usalama [ambao] umeenea katika mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini.” “Mapigano yameongezeka katika mikoa hii katika miezi ya hivi karibuni, na kuwafanya zaidi ya watu 100,000 kuhama makazi yao,” alielezea.

“Idadi ya watu katika kambi hawapati chakula cha kutosha. Kuna magonjwa mengine, na msongamano ni tatizo. Kwa hivyo, tunatoa wito wa mwitikio wa haraka ili kuepusha mkoa huu kwa mlipuko huu wa virisi vya Ebola. Kwanza, kwa kupelekwa kwa wafanyakazi waliobobea. Tunatarajia wafanyakazi hawa kupelekwa haraka iwezekanavyo. Lazima pia tuhakikishe vituo vya matibabu. Rasilimali tulizokuwa nazo zilitengwa kwa ajili ya vita, na vita hivi vya pili ambavyo viko kwa sasa vinahitaji rasilimali zaidi. Mwishowe, tunahitaji pia kuimarisha uwezo wa wafanyakazi wote na timu za uingiliaji kati katika maeneo yote ya afya. Na tunahitaji kuhamasisha rasilimali za kifedha: lazima zipatikane. Kadiri tunavyopoteza muda mwingi, ndivyo tunavyokaribia kushuhudia hali mbaya zaidi ” , alisema Johnny Luboya Nkashama, gavana wa kijeshi wa mkoa wa Ituri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *