Kaizer Chiefs yaachana na Kaze, Mosimane awindwaKaizer Chiefs yaachana na Kaze, Mosimane awindwa

Kaizer Chiefs imetangaza kuachana na makocha wake Cedrick Kaze na Youssef Ben Khalil kuanzia leo Jumanne, Mei 26, 2026.

Klabu hiyo imetangaza kwamba kufuatia kumalizika kwa mikataba ya makocha hao ambao waliongoza timu kwa pamoja baada ya klabu hiyo kuachana na Nasreddine Nabi, Kaze na Youssef hwatoongezewa mikataba mipya.

“Baada ya Nabi kuondoka, wote wawili walipandishwa kukiongoza kikosi cha wakubwa na kuiwezesha timu kumaliza na pointi 54 kwenye ligi ambazo ni matokeo bora ya pili katika kipindi cha miaka 11. Pia walishindwa kuingia hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa wakimaliza na pointi 10 katika kundi D.

“Tunapenda kutoa shukrani zetu kwa makocha hawa kwa mchango na kujitolea kwao na tunawatakia kila la kheri,” imesema taarifa ya Kaizer Chiefs.

Kaze alijiunga na Kaizer Chiefs Oktoba 2024 baada ya ombi la Nabi kwa uongozi wa timu hiyo la kumuongeza raia huyo wa Burundi.

Kwa upande wake Youssef alijiunga na Kaizer Chiefs kbla ya kuanza kwa msimu wa 2024/2025 akiwa pamoja na Nabi.

Wawili hao wameiongoza Kaizer Chiefs kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Afrika Kusini jambo lililoipa tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali Afrika Kusini, Kaizer Chiefs inaonekana kuvutiwa zaidi na Kocha wa zamani wa Al Ahly na Mamelodi Sundowns, Pitso Mosimane ambaye kwa sasa hana timu anayoifundisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *