Kuelekea mashindano ya UMISSETA kwa shule za sekondari, Mkoa wa Manyara umepokea vifaa vya michezo vitakavyotumika kuimarisha us…Kuelekea mashindano ya UMISSETA kwa shule za sekondari, Mkoa wa Manyara umepokea vifaa vya michezo vitakavyotumika kuimarisha us…

Kuelekea mashindano ya UMISSETA kwa shule za sekondari, Mkoa wa Manyara umepokea vifaa vya michezo vitakavyotumika kuimarisha ushiriki wa wanafunzi katika mashindano hayo na kusaidia kukuza vipaji vya michezo mashuleni.

Vifaa hivyo vimetolewa na City College Ilala na kukabidhiwa katika mkutano wa wakuu wa shule za sekondari Kanda ya Kaskazini Magharibi uliofanyika wilayani Mbulu Mei 26, 2026.

Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo, Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Manyara, Mugisha Galibona, amewataka wakuu wa shule kuhakikisha wanavitunza na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kusaidia kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi kupitia michezo.

Akikabidhi vifaa hivyo vya michezo, Mkurugenzi Mkuu wa City College Ilala, Shaban Mwanga amesema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na shule mbalimbali nchini katika kuimarisha sekta ya elimu na michezo kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kufikia ndoto zao kupitia vipaji na taaluma.

Naye Rais wa TAHOSSA Taifa ameipongeza City Institute kwa mchango wake katika kuhamasisha wanafunzi kushiriki michezo pamoja na masomo ya sayansi, akisema hatua hiyo inaonesha uzalendo na dhamira ya kusaidia maendeleo ya elimu nchini.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *