- Mwalimu wa St. Cecilia Misikhu Girls Secondary School alifariki ghafla katika hoteli muda mfupi baada ya kuhudhuria hafla ya shule
- Uchunguzi wa maiti ulifichua chanzo cha kifo cha mwalimu huyo huku kukiwa na wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo
- Katibu mtendaji wa KUPPET aliwahimiza walimu kufanyiwa uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kuzuia majanga kama hayo siku zijazo
Bungoma: Naibu mkuu wa shule ya St. Cecilia Misikhu Girls Secondary School katika eneo bunge la Webuye amefariki dunia.

Source: Facebook
Caleb Wekesa Nasikhu alifariki Jumapili, Mei 24, baada ya kuanguka katika hoteli.
Kulingana na ripoti ya polisi iliyowasilishwa katika Kituo cha Polisi cha Webuye, Wekesa alionekana mara ya mwisho akiwa na mwanamke katika sehemu ya burudani baada ya kuhudhuria hafla ya shule.
Nini kilitokea kabla ya kifo cha Caleb Wekesa?
Mwanamke huyo alidai kuwa alikutana na Wekesa katika SK Club majira ya saa mbili usiku, ambapo walikunywa pombe pamoja na marafiki kabla ya kuelekea Thumbs Club.

Pia soma
Alice Riang’a: Mpenzi wa mwanafunzi wa JOOST aliyeuawa ahudhuria maziko, kihisia aomboleza kwa picha
Inadaiwa kuwa naibu mkuu huyo na mwanamke huyo waliondoka eneo hilo saa saba usiku na kuingia katika Satellite Hotel.
Ripoti ya polisi ilionyesha kuwa mnamo saa sita na dakika ishirini usiku katika siku hiyo ya tukio, marehemu huyo, baba wa watoto wanne, alianza kujihisi vibaya.
Mwanamke huyo aliwaarifu wasimamizi wa hoteli, ambao waliitikia na kumkuta akitokwa na povu mdomoni ndani ya chumba.
Wekesa alikimbizwa katika Hospitali ya Calvary mjini Webuye na wafanyakazi wa hoteli pamoja na mwanamke huyo, kisha akahamishiwa Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Webuye, ambako alifariki takriban dakika 10 baada ya kuwasili. Mwanamke huyo alikamatwa kusaidia polisi katika uchunguzi wao.
“Yeye ni mwanangu wa kwanza. Nilishtuka kusikia kuhusu kifo chake saa kumi alfajiri. Mtu aliyetupigia simu alikuwa mke wake waliyeachana naye miaka miwili iliyopita. Nataka uchunguzi wa kina kuhusu tukio hili,” alisema babake.
Familia ilidai kuwa Wekesa hakuwa na historia yoyote ya matatizo ya kiafya.

Source: Facebook
Nini kilimuua mwalimu Caleb Wekesa?
Kulingana na katibu mtendaji wa KUPPET Augustine Kundu Luketelo pamoja na mke wa Wekesa, uchunguzi wa maiti ulionyesha kuwa mwalimu huyo alifariki kutokana na “mshtuko wa moyo uliopasuka” uliosababishwa na shinikizo.
“Tunasikitika sana kumpoteza mwalimu wetu. Uchunguzi wa maiti unaonyesha alikufa kutokana na presha. Kwa niaba ya familia yangu na walimu wa Bungoma, ninatoa pole zangu kwa familia iliyofiwa.
Pia nataka kuwafahamisha walimu, ambao hufanya kazi nyingi, kwamba saratani, kisukari, na presha ni mambo ya kawaida sana. Nawahimiza walimu kufanyiwa vipimo mara kwa mara ili kudhibiti hali hizi,” alisema Luketelo.
“Nilimkuta akiwa na karatasi iliyoandikwa ‘dead on arrival.’ Ameniacha na watoto wanne wadogo. Ripoti inaonyesha alikufa kutokana na mshtuko wa moyo. Ninamuomboleza mume wangu. Aache apumzike kwa amani,” aliongeza mke wake wa miaka 20.
Mwalimu mkuu wa shule ya Ratanga Girls afariki
Katika habari nyingine, mwalimu mkuu wa shule ya Ratanga Girls Secondary School Mildred Ngesa alifariki dunia, jambo lililoiacha jamii ikiwa katika huzuni kubwa.
Video iliyosambazwa mtandaoni ilionyesha wanafunzi wakiwa katika majonzi makubwa wakimuomboleza Ngesa, ambaye hakuwa tu mwalimu, bali pia mshauri, mama, na mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wote pamoja na wale waliomzunguka.
Mbunge wa Ndhiwa Martin Owino alifichua kuwa mkuu huyo wa shule aliyefariki alitoa mchango mkubwa katika sekta ya elimu, akibainisha kuwa urithi wake utakumbukwa milele.

Pia soma
“Starehe Iliyokatiza Maisha!”: Jamaa wa Miaka 50 Afariki Kichakani Uganda Akirusha Roho na Demu
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke

