Ulaya Magharibi inajiandaa kwa siku nyingine ya joto kali kwa mwezi MeiUlaya Magharibi inajiandaa kwa siku nyingine ya joto kali kwa mwezi Mei

Kuanzia Uingereza hadi Italia, sehemu za Ulaya zinajiandaa leo Jumanne kwa siku nyingine ya joto kali kwa mwezi Mei, na kuvuruga utaratibu katika bara ambalo linapata joto haraka zaidi kuliko mahali pengine popote.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Vizuizi vya kazi za nje vilivyowekwa nchini Italia, fukwe zilizojaa watu nchini Ufaransa licha ya kutokuwepo kwa walinzi wa uokoaji, mavuno ya mapema kwa wakulima… Halijoto imekuwa ikiongezeka kwa siku kadhaa, na kusababisha rekodi za juu ya 30°C mapema siku ya Jumatatu nchini Uingereza na Ufaransa.

Siku ya Jumatatu ilikuwa siku yenye joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa kwa kipndi cha mwezi Mei nchini Ufaransa, kulingana na Mamlaka ya hali ya hewa nchini Ufaransa, Météo-France.

“Kuba la joto” 

Jambo hili husababishwa na mtiririko wa hewa ya moto kutoka Afrika Kaskazini ambayo hukwama chini ya shinikizo kubwa la kimbunga chenye nguvu. Kulingana na makubaliano ya kisayansi, mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na binadamu hufanya matukio mabaya ya hali ya hewa kama vile mawimbi ya joto, ukame, na mafuriko kuwa makali zaidi.

Kutokana na “kuba hili la joto,” kipimo cha joto kilipanda hadi 34.8°C kwa mara ya kwanza Jumatatu katika Bustani za Kew, bustani ya mimea iliyoko kusini magharibi mwa London. Hii ilizidi rekodi ya awali ya mwezi Mei, ambayo ni ya tangu mwaka wa 1944, kwa 2°C, ikizidi kwa mbali kiwango cha kawaida cha 17 au 18°C.

“Joto kama hilo lilikuwa kali nchini Uingereza katikati ya kiangazi,” imebainisha Ofisi ya Met, ambayo inatarajia halijoto kama hiyo leo Jumanne kabla ya kushuka hadi karibu 20°C mwishoni mwa wiki. Ireland pia ilipitia halijoto iliyovunja rekodi mwezi Mei, ikifikia 28.8°C kusini.

Rekodi ya joto nchini Ufaransa kwa mwezi Mei

Nchini Ufaransa, pamoja na rekodi ya joto ya kitaifa kwa mwezi Mei siku ya Jumatatu, rekodi kadhaa za ndani zilivunjwa, kulingana na Météo-France, ikiwa ni pamoja na 34.3°C huko Nantes (magharibi) na 34.7°C huko Bergerac (kusini magharibi). Mamlaka ya hali ya hewa ilitoa onyo la wimbi la joto la rangi ya chungwa usiku, la pili kati ya viwango vitatu vya tahadhari, kwa maeneo manane magharibi mwa Ufaransa, tukio ambalo halijawahi kutokea mapema mwaka huu. Wimbi la joto linatarajiwa kuongezeka leo Jumanne, huku viwango vya juu vya 36°C vikitarajiwa katika maeneo haya. Inatarajiwa kudumu hadi mwisho wa wiki, kulingana na chanzo hicho.

Nchini Uhispania, Mamlaka ya hali ya hewa zilionya kuhusu usiku wa kitropiki ulioenea kusini-magharibi kuanzia Jumatano na kutabiri kilele kati ya Jumatano na Ijumaa na viwango vya juu vya 36-38°C.

Nchini Italia, katika eneo la Lazio ambalo linajumuisha Roma, kanuni inayoweka kikomo cha kazi “kwa kuathiriwa na jua kwa muda mrefu” kati ya saa 6:30 mchana na saa 10:00 alaasiri ilipitishwa Jumatatu. Sheria hii ilianzishwa mwaka jana mnamo Mei 30, na inatumika hadi Septemba 15.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *