Mchezaji wa soka wa Nigeria, Victor Udoh, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 21 mjini Abuja nchini Nigeria, katika mazingira…Mchezaji wa soka wa Nigeria, Victor Udoh, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 21 mjini Abuja nchini Nigeria, katika mazingira…

Mchezaji wa soka wa Nigeria, Victor Udoh, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 21 mjini Abuja nchini Nigeria, katika mazingira yanayochunguzwa na mamlaka za nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za vyombo vya habari vya kimataifa, nyota huyo wa zamani wa klabu za Southampton ya Uingereza na Royal Antwerp ya Ubelgiji alikutwa amefariki baada ya kuripotiwa kutoka na marafiki zake usiku mmoja kabla ya tukio hilo.

Ripoti za awali zinaeleza kuwa chanzo cha kifo bado hakijathibitishwa rasmi, ingawa baadhi ya taarifa zinadai huenda kulikuwa na tukio la sumu ya chakula au kinywaji wakati ambao Uchunguzi unaendelea kubaini ukweli wa tukio hilo.

Victor Udoh alikuwa mmoja wa vipaji vilivyokuwa vikitarajiwa kung’ara katika soka la Ulaya baada ya kucheza katika timu za vijana za Royal Antwerp kabla ya kujiunga na Southampton mwaka 2025, na baadaye kuhamia klabu ya Dynamo České Budějovice ya nchini Czech Republic.

Vilabu vya zamani alivyopita mchezaji huyo pamoja na mashabiki wa soka duniani vimetuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huo mkubwa.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *