
Chama kikubwa zaidi cha wanafunzi nchini Senegal (UGEB), kimesitishwa kwa miezi mitatu, na viongozi kadhaa, ambao idadi yao haijafichuliwa, wamekamatwa na kupelekwa mahali pasipojulikana. Sababu: taarifa iliyotolewa Mei 19, ambapo chama hicho kililaani ukosefu wa maendeleo katika mapambano dhidi ya ugaidi nchini humo, licha ya upatikanaji wa vifaa muhimu vya kijeshi. Taarifa hizi hazikupendeza mamlaka, ambayo ilieleza kutofurahishwa kwake.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ilikuwa wakati wa maadhimisho ya miaka 36 ya mauaji ya mwanafunzi Dabo Boukary chini ya utawala wa Blaise Compaoré ambapo chama hiki cha wanafunzi kilishutumu utawala wa kijeshi ‘hautoweza kurejesha usalama,” licha ya ahadi zilizotolewa na Kapteni Ibrahim Traoré alipochukua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi.
Siku chache baada ya tangazo hili, watu “wasiojulikana” waliovaa nguo za kiraia wakijihami kwa silaha waliwakamata wanafunzi, akiwemo kiongozi wa UGEB, kwa kutumia “nguvu nyingi na kinyume cha sheria”, kulingana na taarifa kutoka kwa chama hiki cha wanafunzi.
Kufuatia hili, mwendesha mashtaka wa Burkina Faso, katika Mahakama Kuu ya Ouaga 2, alitangaza kufunguliwa kwa uchunguzi wa kimahakama kutokana na “uzito” wa matukio hayo.
Kulingana na taarifa ya mwendesha mashtaka, vitendo vinavyodaiwa vinaweza kuwa makosa yaliyoainishwa na kuadhibiwa chini ya kanuni ya jinai ya Burkina Faso, na vinaweza kuchukuliwa kama jaribio la “kuvikatisha tamaa vikosi vya ulinzi na usalama.”
Mwendesha mashtaka alibainisha kwamba “kuunga mkono hadharani vitendo vya ugaidi” kunaadhibiwa kwa kifungo cha mwaka mmoja hadi kumi jela.
