Mazungumzo ya usalama kati ya Israel na Lebanon yanaanza WashingtonMazungumzo ya usalama kati ya Israel na Lebanon yanaanza Washington

 Sehemu ya usalama ya mazungumzo kati ya Israel na Lebanon yanaanza leo Ijumaa Mei 29 huko Washington, nchini Marekani, chini ya usimamizi wa utawala wa Trump, wakati mapigano yakiendelea kushika kasi nchini Lebanon, hali ambayo inafanya usitishaji mapigano uliopo tangu Aprili 17 kutokuwa na maana. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Lengo la majadiliano kati ya wawakilishi wa usalama wa Lebanon na Israel ni kuunda mazingira yanayofaa kwa mazungumzo ya kisiasa ambayo yataanza tena wiki ijayo kati ya nchi hizo mbili. Lakini madaia ya Marekani yanaonekana kuwa magumu kwa upande wa Lebanon kuyatimiza.

Sehemu hii ya usalama ya majadiliano, tofauti na sehemu ya kisiasa inayotarajiwa wiki ijayo, ilianzishwa na utawala wa Trump. Kulingana na vyombo vya habari vya Marekani, Washington ingependa kuendelea na suluhisho la kiufundi na jeshi la Lebanon: kuundwa kwa kitengo kilichojitolea mahsusi kwa ajili ya kupokonya silaha Hezbollah. Wazo hili haliungwi mkono kwa kauli moja nchini Lebanon, kwani lina hatari kubwa za kisiasa.

Kugawanya jeshi la Lebanon kunaonekana sana kama hatari kwa taifa zima. Makabiliano ya moja kwa moja na Hezbollah yenye vifaa bora zaidi yanaonekana kama kujiua. Chama kinachomiliki wanamgambo hawa wala mshirika wake wa Kishia Amal hawajatuma mwakilishi kwenda Washington.

Hezbollah na chama cha Amal wapinga

Wanakataa wazo la mazungumzo ya moja kwa moja na Israel, ambayo, haswa wiki hii, iliimarisha operesheni zake za kijeshi kusini mwa Lebanon, rasmi ili kuzuia ndege zisizo na rubani za Hezbollah kufika kaskazini mwa Israel. Ujumbe wa Lebanon utaweka kipaumbele katika usitishaji mapigano wa kweli, kamili na kuondolewa kwa jeshi la Israel kutoka eneo linalokaliwa.

Katika kuunga mkono ombi lake, ujumbe wa Lebanon unakumbusha hasara kubwa ya vifaa na vifo vya binadamu kutokana na mashambulizi ya Israel nchini humo tangu Machi 2, ambapo zaidi ya watu 3,000 waliuawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *