Chama cha mapinduzi CCM mkoani Tabora, kimehitisha kampeni za uchaguzi mdogo katika Kata ya Itilo wilayani Nzega na Kata ya ziba Wilayani Igunga, huku kikiwaomba wananchi kuwachagua wagombea wa chama hicho kwa kuwa CCM imeendelea kutekeleza ahadi zake za maendeleo na haitasita kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), uchaguzi mdogo wa kesho unahusisha uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Isimani mkoani Iringa pamoja na uchaguzi wa madiwani katika kata 12 za Tanzania Bara, zikiwemo Kata ya Itilo wilayani Nzega na Kata ya Ziba wilayani Igunga mkoani Tabora kufuatia vifo vya waliokuwa viongozi katika nafasi hizo.

Hata hivyo katika Kata za Itilo Nzega CCM inawakilishwa na ndugu Michael Kasinza huku kata ziba ikiwakilishwa na Themistoles Emilian.

@deilahmomo

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *