Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, , amesema baadhi ya watu wanaobeza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali wanapaswa kuombewa ili watambue mchango wa miradi hiyo katika kuboresha maisha ya wananchi.

Kihongosi ameyasema hayo leo Mei 31, 2026, wakati wa ziara yake katika Tawi la Bomani, Shina Namba 1 la CCM, Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, iliyolenga kukagua uhai wa chama na kuimarisha shughuli za kisiasa katika ngazi za mashina na matawi.

Amesema kumekuwepo na baadhi ya watu wanaodharau mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kudai kuwa ujenzi wa barabara za lami si maendeleo, jambo alilosema linaonesha kutotambua umuhimu wa miradi hiyo kwa wananchi.

Aidha, amewataka wananchi wa Wilaya ya Hai kuendelea kuiunga mkono Serikali na kupuuza kauli zinazolenga kubeza maendeleo yanayotekelezwa nchini, akisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, , miradi mingi ya maendeleo imeendelea kutekelezwa na kuwanufaisha wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *